Masama Blog


Muda Wapita Tena Bila Jammeh Kuondoka Madarakani Gambia

Jammeh alikuwa ameomba apewe hadi saa 16:00 (saa moja jioni Afrika Mashariki) kufanya uamuzi kuhusu iwapo ataachia madaraka au la.

Makataa ya kwanza ya kumtaka aachie madaraka kufikia saa sita mchana yalikuwa yamepita.

Taarifa zinasema makamu wa rais wa zamani wa Gambia, Isatou Njie-Saidy, yupo ikulu ambapo anashiriki mazungumzo ya dakika za mwisho.

Marais wa Mauritania na Guinea wanajaribu kumshawishi Jammeh kuondoka.

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA MABALOZI WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Mabalozi sita aliowateua jana kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali na kuwapa maagizo ya kuitangaza vema na kuiletea maendeleo Tanzania.

aHafla ya kuapishwa kwa Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza baada ya Mabalozi hao kula viapo vyao, Rais Magufuli amewataka kuiwakilisha vizuri Tanzania katika nchi walizopangiwa kwa kuhakikisha wanasimamia maslahi ya Tanzania.
“Nendeni mkatekeleze kazi zenu kwa upendo mkubwa mkijua umma wa Watanzania upo nyuma yenu, Maslahi ya Watanzania yakawe mbele, Tanzania kwanza ikawe mbele, na mimi nina uhakika mtakuwa mmewafanyia Watanzania mema na mazuri sana”
Rais Magufuli akizungumza na mabalozi baada ya kula viapo
“Ukiona kizuri chochote kwaajili ya Watanzania kilete, mkatetee Tanzania, mkajenge uchumi wa Tanzania, mkaimarishe mahusiano ya Tanzania, mkajenge urafiki wa Watanzania, mkajenge biashara za Watanzania” 
Mabalozi walioapishwa ni Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi -Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. James Alex Msekela - Baloziwa Tanzania Geneva - Umoja wa Mataifa, Mhe. Mbelwa Brighton Kairuki - Baloziwa Tanzania nchini China, Mhe. Fatma Mohamed Rajab - Baloziwa Tanzania nchini Qatar, Mhe. George Kahema Madafa - Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mhe. Prof. Elizabeth Kiango Kiondo - Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.
Rais Magufuli akimuapisha Mhe. Prof. Elizabeth Kiango Kiondo - Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.
Wakati huo huo
Baada ya kula kiapo cha Uadilifu, Mhe.Jaji Mstaafu Harold Reginald Nsekela ameongoza kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kwa Mabalozi sita walioapishwa leo kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

MWANA FA: HAKUNA UWEZEKANO WA KUIRUDISHA EAST COAST KAMA KUNDI

Kama inavyoeleweka kuwa game ya music kwasasa ime-change tena kwa kiasi kikubwa sana, kiasi kwamba baadhi ya vitu vilivyo kiki zamani kushindwa kuchukua nafasi kwasasa.

Tume washuhudia mastaa kibao ambao waliumiza kinoma noma hapo awali lakini hali imekuwa ngumu kwa wao kurudi kwenye mstari kwasasa, kutokana na hali ya muziki jinsi ilivyo, muziki ambao unahitajika kwenye soko la sasa na vitu kama hivyo.
Moja kati ya vitu ambavyo vilikuwa vina-shine kinoma noma kipindi cha nyuma ni muziki wa makundi. Ikiwa tuliyashuhudia makundi kibao kama East CoastTMK Wanaume Family na mengineyo kibao yakifanya vizuri sana katika game na kuleta ushindani wa hali ya juu.
Lakini hali imebadilika kwa kiasi kikubwa sana siku hizi na kupelekea makundi kupotea kabisa katika ramani ya music. japo kuwa yapo machache ambayo bado yenaendelea kufanya lakini sio kwa nguvu ile kama ilivyokuwa hapo awali.
Perfect255 imepiga story na Mwana FA ikiwa ni mmoja wa wasanii ambao walikuwa chini ya kundi la East Coast na kutaka kujua mipango yake katika kurudi kufanya muziki wa kundi kwa soko la sasa, na alikuwa na haya ya kusema.
“Nafkiri tunaweza kufanya kazi kwa pamoja, yaani watu wawili, watatu hadi wanne lakini kutengeneza group as a group kwa uchumi wa kimuziki ulivyo sasa hivi itakuwa ni kazi kubwa kidogo. Tunaweza kufanya group ya project, kama tunataka kufanya project hii tukaifanya mwanzo hadi mwisho ikimalizika kila mtu akashika hamsini zake, lakini hakuna uwezekano wa kutengeneza group na ikafanya kazi kama group moja kwa moja, muziki wa group ulisha shindwa.”

Play hii video hapa chini kumsikiliza Mwana FA akifunguka mwanzo hadi mwisho na kiufafanuzi zaidi kuhusiana na suala hilo.

MUIMBAJI WA WIMBO WA "LAMBADA" AKUTWA AMEKUFA KATIKA GARI

Loalwa Braz akiwa na Akon backstage mwaka 2012 kwenye tuzo za Billboard Latin Music Awards, Miami, Florida

Muimbaji wa Brazil, Loalwa Braz, aliyejipatia umaarufu kwa wimbo wake wa mwaka 1989 ‘Lambada’, amekutwa amefariki kwenye gari iliyoungua moto mjini Rio de Janeiro.


Mwili wa muimbaji huyo aliyekuwa na miaka 63 ulikutwa karibu na nyumbani kwake huko – Saquarema.
Polisi bado hawajaweza kutambua sababu ya kifo chake.

Braz alikuwa muimbaji mkuu wa kundi Kaoma lililokuwa na makazi Ufaransa na Brazil na , lililopata umaarufu kwa wimbo Lambada. Msanii wa Marekani, Jennifer Lopez aliwahi kusample wimbo huo kwenye hit yake ya mwaka 2010, On The Floor.

Wizara zote zatakiwa Kuhamia Dodoma kabla ya Feb. 28

Serikali imezipa msisitizo wizara mbalimbali kuhakikisha zinahamishia makazi yake Makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma kabla ya Februari 28, mwaka huu, kama ilivyotangazwa na Rais John Magufuli mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema agizo la serikali lazima liwe limetekelezwa ifikapo Februari 28, mwaka huu.

“Kama agizo lilivyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wizara na watumishi wake kuhamia Makao Makuu Dodoma, ndivyo wanavyotakiwa manaibu makatibu wakuu, makatibu, manaibu mawaziri na mawaziri kutakiwa kuwapo Dodoma mwishoni mwa Februari,” alisema Mhagama.

Waziri Mhagama alisema ofisi yake imeweza kukagua miundombinu na ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali yanayoendelea kujengwa na mengine yakiwa yamekamilika kwa ajili ya matumizi ya wizara hizo.

“Hakuna tatizo la ofisi za watumishi wa wizara zote, kwani majengo yamekamilika na yapo katika hali nzuri tayari kwa ajili ya kuanza kutumiwa, hivyo wakuu husika wakiwamo mawaziri wahakikishe wanatakiwa kuhamia Dodoma,” alisema.

Kiongozi wa CHADEMA Apewa Kipigo na Vijana wa CCM Kwa Kuingilia Mkutano wao

Katibu wa Chadema Jimbo la Sengerema, Deusdeth Mwigala juzi, alipata kipigo kutoka kwa vijana wa CCM kilichosababisha apoteze fahamu baada ya kutuhumiwa kutaka kuvuruga mkutano wa hadhara. 

Kiongozi huyo wa Chadema alikuwa akipita karibu na eneo ambalo CCM walikuwa wakiendelea na mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kahumulo, akiwa na vipaza sauti alivyotumia kutangaza mkutano wa chama chake, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kuvuruga usikivu.

Hata hivyo, katibu huyo alikana kuvuruga mkutano wa chama hicho akidai alikuwa umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka eneo ambalo CCM ilikuwa ikiendesha mkutano.

“Wakati naendelea na kazi ya kutangaza mkutano wa Chadema nikiwa nimeongozana na makada wengine wanne na dereva, ghafla tulivamiwa na watu wa CCM na wakaanza kutushambulia,” alisema Mwigala akizungumzia tukio hilo lililotokea Kijiji cha Lubanda.

Alisema wenzake pamoja na dereva walifanikiwa kukimbia, lakini yeye alinaswa na wafuasi hao walioendelea kumshambulia kwa kipigo. 

Hata hivyo, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, James Kisinza alimtupia lawama katibu huyo wa Chadema kwa kitendo cha kupita karibu na eneo la mkutano wa CCM akitangaza mkutano wa chama chake kwa kutumia vipaza sauti na hivyo kuvuruga usikivu. 

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Sengerema, Hassan Moshi alisema wafuasi wao walichukizwa na kitendo hicho na kuamua kumuadhibu kiongozi huyo kwa madai kuwa alikuwa anavuruga mkutano wao kwa makusudi. 

“Viongozi tulilazimika kuingilia kati kumwokoa asiendelee kuadhibiwa na vijana wenye hasira, lakini ukweli ni kwamba mwenzetu alifanya kosa kwa kuingilia mkutano wa chama kingine kinyume cha sheria,” alisema Moshi. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema ofisi yake haijapokea taarifa hizo na kuahidi kuzitolea ufafanuzi baada ya kuzipokea kutoka Sengerema.

Msajili wa Vyama Ashikilia Msimamo wake Wa Kumtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema hana hofu ya kuchafuliwa kutokana na tuhuma zinazotolewa dhidi yake, huku akisema msimamo wake uko palepale na kwamba anamtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif ni Katibu Mkuu.

Kauli ya Jaji Mutungi imekuja baada ya taarifa na kauli za matusi na kejeli zilizomuhusisha yeye na ofisi yake kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya kuidhinisha zaidi ya Sh300 milioni za ruzuku kwenda kwenye akaunti ambayo kamati ya uongozi ya CUF ilidai siyo ya chama hicho.

Taarifa za msajili kuingiza fedha hizo kwenye akaunti hiyo na baadaye kutolewa kwa njia ambayo inaonekana kutia shaka zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ambaye alilinganisha suala hilo na uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Kupitia taarifa yake jana, Jaji Mutungi alisema kuna mbinu zinazopangwa na wanaojiita Kamati ya Uongozi ya CUF ambayo ofisi yake haiitambui, huku akisisitiza kumtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif kuwa Katibu Mkuu.

Jaji Mutungi ambaye mwishoni mwa mwaka jana alifunguliwa kesi Mahakama Kuu na bodi ya wadhamini wa CUF ikiiomba itoe amri ya kubatilisha barua ya mlezi huyo wa vyama vya siasa inayomtambua Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF, alisema kauli zinazotolewa mitandaoni zina lengo la kuchafua ofisi yake.

“Tayari mbinu hizo zimeanza kutekelezwa na viongozi wa kamati hiyo kwa kusambaza habari za kudhalilisha katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kama Facebook na mingineyo,” alisema. 

Msajili huyo alisema moja ya mkakati huo ni taarifa iliyosambazwa juzi na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF,, Mbarala Maharagande ya kejeli, matusi, tuhuma na dhihaka kwake.

Jaji Mutungi alisema hivi karibuni, Maharagande alizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ofisi ya msajili inasababisha mpasuko ndani ya chama hicho na ndiyo maana imetoa ruzuku kwa Profesa Lipumba.

Licha ya tuhuma hizo, Jaji Mutungi alisema kwamba haogopi kuchafuliwa akizingatia ukweli kwamba yeye ni mtumishi wa umma na anafanya kazi zake akiwatumia wananchi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema kamwe hawezi kuyumbishwa na matusi wala kejeli zinazotolewa dhidi yake pamoja ofisi anayoiongoza.

“Nimezipata hizo taarifa kwamba kuna baadhi ya watu wamepanga kupambana nami kwa kunichafua, japo naendelea kuzifanyia kazi lakini waache wanichafue, wala siogopi lolote,” alisema. 

Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema mjadala wa ruzuku ya CUF aliyotoa kwa chama hicho ameshaufunga na anashangazwa na maneno yanayozidi kusambazwa na watu wanaojiita viongozi wa CUF.

Alipotafutwa  kuzungumzia tuhuma hizo, Maharagande aliendelea kusisitiza kuwa kauli iliyotolewa wakati alipofanya mkutano na vyombo vya habari ipo hivyo na kwamba waliitisha mkutano kumjibu msajili ambaye alifanya mkutano na waandishi wa habari siku moja kabla kuhusu masuala ya CUF. 

Mahakama Yaridhia Umeya wa Mtoto wa Marehemu Sitta Manispaa ya Kinondoni..!!!Soma yote hapa ilivyokuwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtambua Benjamin Samweli Sita (pichani) kuwa meya wa Kinondoni. Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa pili Ukawa waliofungua kesi kupinga matokeo ya ushindi huo.

Itakumbukwa kuwa, siku ya uchaguzi huo, polisi waliwakamata baadhi ya viongozi na wajumbe wa UKAWA sambamba na ongezeko la wajumbe batili upande wa CCM.

CHADEMA na Ukawa walifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupinga ushindi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta huku walalamikaji wakiwa ni Mustapha Muro (aliyekuwa mgombea Meya Manispaa ya Kinondoni) na Jumanne Amir Mbunju (aliyekuwa mgombea Naibu Meya wa Manispaa hiyo) wote wakiwakilisha na Wakili wa CHADEMA, John Malya.

Kesi iliyofunguliwa dhidi ya Afisa Utawala wa Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Samweli Sita (aliyetangazwa kuwa Meya) na Manyama Mangaru (aliyetangazwa kuwa Naibu Meya).

ANGALIA MAANDALIZI YA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE DONALD TRUMP

Billedresultat for TRUMP INAUGURATION PREPARATION
Maandalizi ya kuapishwa Rais mteule Donald Trump yakiendelea siku mbili zilizopita tayari kwa kuapishwa siku ya kesho Ijumaa Januari 20, 2017.
Billedresultat for TRUMP INAUGURATION PREPARATION
Mafundi wakiweka mambo sawa.

Billedresultat for TRUMP INAUGURATION PREPARATION
Wapiga picha za kuganda na video wakifanya maandaliza na majaribio ya picha na video zitkavyokua.
Billedresultat for TRUMP INAUGURATION PREPARATION
Ujenzi ukiendelea.
Billedresultat for TRUMP INAUGURATION PREPARATION
 

Safi Sanaa!! Wanafunzi wa Diploma Eti nao Watapewa Mikopo,Soma Hapa Livee..!!!


SERIKALI imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua elimu husika.


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mabadiliko hayo, yamelenga kuwezesha kasi katika uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako alisema mabadiliko katika Sheria Namba 4 ya Mwaka 2016 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), yamelenga kutoa nafasi ya kada ya Stashahada inayohitajika ambao wamekuwa hawapati mikopo.

“Kwa lengo la kupata balance (mizania) na kwa kuwa Diploma nayo iko kwenye elimu ya juu, watoto ni wale wale. Kuna wengine nao wanashindwa kumudu gharama na ili serikali ipate uwiano mzuri tumeona ni vizuri kuwe na marekebisho ya sheria,” alieleza Profesa Ndalichako.

Profesa Ndalichako alisema kuna umuhimu mkubwa wa kada ya Stashahada, hasa wanaokwenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa kwenye msukumo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa ujenzi wa taifa la vijana, kama ilivyo kwa wenye Shahada.

“Kama taifa tunazungumzia uchumi wa viwanda,wadau wote hata wale wa ngazi ya kati ni muhimu katika kuhakikisha kwamba ajenda hii inafanikiwa kama vile ambavyo wale wa digrii wangelifanya,” aliongeza waziri huyo.

Mwaka 2004, kulikuwepo na mabadiliko katika sheria hiyo iliyowezesha wanaochukua masomo ya sayansi, hisabati na elimu ya msingi (kwenye msisitizo wa sayansi na hisabati), kupata mikopo ya elimu, nafasi iliyoanza kutumika mwaka 2014, lakini hatua hiyo ilisimamishwa wakati wa muhula wa masomo wa mwaka 2016/17.

Hata hivyo, HESLB ilikaririwa ikisema kwamba maamuzi ya kusitisha utoaji wa mikopo, ililenga kutekeleza maagizo ya serikali. Hata hivyo, jana Profesa Ndalichako alisema kwamba uamuzi wa kusimamisha mikopo hiyo,ulitokana na nia ya serikali kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ili kuipa wigo mpana zaidi kuliko kujikita katika eneo la sayansi pekee.

“Mwaka 2004 tuliingiza diploma, lakini kwa masomo ya sayansi pekee sasa, tunataka kuwa na kipengele kinachopanua wigo ili tuweze kuhusisha kozi nyingine za diploma ambazo zinaenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa,” alifafanua waziri huyo.

Kwa mwaka wa masomo 2016/17, serikali ilipanga bajeti ya Sh bilioni 483 ambazo zitakopeshwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea. Katika mwaka huo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo walikuwa ni 25,715.

Wakichangia mjadala huo, Mbunge wa Malindi, Ally Saleh (CUF) alitahadharisha kuhusu vipaumbele vya kitaifa na kutaka kuwapo na ufafanuzi ili kuondoa utata. “Sijafurahi sana na phrasing of national priority.

Naogopa isije ikajibana au ikatumika katika hali itakayoleta utata. Hivi karibuni tulikuwa na utata mkubwa wa nani apewe mikopo...sasa tunasikia kuwa tunaenda kwenye uchumi wa viwanda isije fedha zote zikapelekwa kule.

“Kutafutwe njia ya kudetermine hizo priority za kitaifa na kujua watakuwa wangapi ili tujue kichumi itagharamu kiasi gani ilitusishindwe huko mbele,” alisema Saleh.
 
Fikra ya kutanua wigo kwa wanafunzi wa Stashahada ilifafanuliwa na watu wa Bodi ya Mikopo kwamba imezingatia kuwa katika sekta zote kutatakiwa uwiano wa wataalamu wa kada mbalimbali. Aidha, imeelezwa kuwa waziri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wataweza kushauriana na kuona hitaji ya kada mbalimbali zinavyokwenda.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MAKAMBAKO KUANZA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na ULinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe baada ya kuwasili Makambako kuanza ziara ya mkoa huo Januari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maua kutoka kwa Skauti baada ya kuwasili Makambako kuanza ziara ya mkoa wa Njombe Januari 19, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Christopher Ole Sendeka. (Picha na Ofisi ya Wiri Mkuu)