Ticker

10/recent/ticker-posts

Kaizer Chiefs Wanamtaka Kocha Gamondi, Mkataba wake Yanga ..Soma hapa

 Kaizer Chiefs Wanataka Kocha Gamondi, Mkataba wake Yanga Wamalizika Karibuni

Inaelezwa wakati Yanga ilipokuwa Sauzi ikicheza na Mamelodi Sundowns, klabu kubwa ya huko Kaizer Chiefs ilikuwa inapiga hesabu ikiwa jukwaani na fasta ikalichukua jina la kocha wa wababe hao wa Ligi Kuu Bara, yaani Miguel Gamondi.

Kaizer Chiefs maarufu kama Amakhosi wamelichukua jina la Gamondi katika mchujo wa mwisho baada ya kushusha sapraizi bab’kubwa ya kuwabana Mamelodi nyumbani baada ya awali kuwabana Kwa Mkapa jambo liiliwashtua mabosi wa Kaizer wakiona kama kocha huyo Muargentina anaweza kuja kuwa suluhisho la kusitisha ufalme wa Mamelodi katika Ligi ya PSL.

Hatua ya kushtua zaidi kwa Yanga ni Gamondi mkataba wake na Yanga umebakiza miezi tu kabla ya kumalizika mwisho wa msimu huu, kitu kilichowaongezea mzuka mabosi wa Kaizer kuliweka jina lake mezani. Kama mnakumbuka wakati Yanga inarejea kutoka Afrika Kusini, Gamondi alishtua zaidi alipozungumza kwa kusema bado hana uhakika kama ataendelea na Yanga kwa msimu ujao, kauli iliyoongeza presha kwenye mustakabali wa kocha huyo klabuni hapo.

Post a Comment

0 Comments