Msajili wa Hazina Tanzania, Nehemiah Mchechu, amewaagiza Wenyeviti wa Bodi za Taasisi za umma kuandaa mipango ya kurithisha nafasi tatu muhimu za uongozi ndani ya asasi zao.
Mchechu alisisitiza kuwa bila mipango hiyo, mamlaka za uteuzi mara nyingi huchagua viongozi kutoka nje yaTaasisi, ambao wanaweza kukosa uzoefu muhimu.
Bwana Mchechu ameyasema hayo wiki iliyopita Julai 15, 2024 wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Kongamano la Wakurugenzi Watendaji lililofanyika jijini Arusha.
Mchechu alieleza kuwa mipango hiyo ya urithi inapaswa kuundwa na bodi na kujumuisha wagombea wasiopungua watatu