Ticker

10/recent/ticker-posts

Duuh..Kumbe hii ndio simu anayotumia Waziri Jerry Silaa


Kama wengi mnavyokumbuka siku ya Kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka Mbunge wa Ukonga ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa alikuwa mmoja wa waalikwa waliosali kanisani kwa mtume  na nabii Suguye lililopo Kitundu Ukonga Jijini Dar es Salaam.Moja ya mambo yaliyozua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii ni aina ya Simu anayotumia waziri silaa tofauti na wengi walivyotarajia huku waki sema  mengi juu ya simu hiyo iliyoonekana pia kuwa tofauti na simu za viongozi na watu wenye majina makubwa kama ilivyozoeleka na wengi.
Baada ya kufatilia kwa kina na kujiridhisha imegundulika kuwa Mhe.Silaa anatumia simu ya kawaida kabisa aina ya Techno ambazo kwa sasa watu wengi wanachkukulia kwamba ni simu za watu wa hadhi ya chini jambo ambalo Mhe.Silaa amepinga na kusema yeye ni  mpenzi na muumini wa simu za bei ya kitanzania na kizalendo kwani yeye a naamini kikubwa ni mawasilano na siyo aina ya simu kitu ambacho wengi wamefurahishwa na kauli hiyo 
Katika ibada hiyo pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Samia Suluhu Hassan alimpigia simu Nabii Suguye kupitia simu ya Waziri  Jerry Silaa na kumpongeza Nabii Suguye kwa Kazi ya Mungu anayoifanya,Pia waziri Silaa alitumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania wamuombee Rais Samia kwa Kazi Kubwa anayoifanya kwa Taifa na watanzania kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments