Ticker

10/recent/ticker-posts

RC Rosemary Senyamule afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi PPRA

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amefungua mkutano wa Nne wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya udhibiti na ununuzi wa Umma (PPRA) Leo tarehe 24 Aprili 2024 katika ukumbi wa Mamlaka wa PPRA Jijini Dodoma.

Mkutano huo una lengo la kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano na kuongeza ufanisi katika kazi.

Katika mkutano huo uliowasilisha hoja ya shughuli zilizopangwa kufanyika ikiwemo taarifa za utekelezaji wa majukumu ya idara na vitengo vya Mamlaka kwa Mwaka 2023/2024 Kwa kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Machi 2024 pamoja na mwelekeo wake kwa mwaka 2024/2025.

Pia Mkutano huo umejadili taarifa ya mpango wa bajeti inayopendekezwa kwa waka 2024/2025 Pamoja na masuala ya watumishi kutoka TUGHE.



Post a Comment

0 Comments