Ticker

10/recent/ticker-posts

Niyonzima Atoa ya Moyoni: Yanga Hii Wataitungua Al-Merreikh Nje Ndani

 Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amesema kuwa ameitazama timu ya Yanga inavyocheza kwa sasa ipo kwenye ubora wa hali ya juu sana kuliko Al-Merreikh ya Sudan.

Niyonzima ambaye amecheza Yanga kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa kabla ya kwenda Simba Sc kisha kurejea tena Yanga kabla ya kurejea kwao Rwanda.

"Ni matumaini yangu makubwa kuwa klabu hii itaifunga Al-Merreikh nje ndani kutokana na ubora walionao Yanga Sc kwa sasa matumaini hayo ninayo kwa asilimia mia na mchezo huo sito ukosa nitautazama," amesema Niyonzima.

Yanga imefanya usajili wa wachezaji kadhaa ambao mpaka sasa wameonekana kufanya vizuri ndani ya timu hiyo huku wakigawa dozi ya bao 5 katika mechi tatu mfululizo.

Septemba 16, 2023 Yanga watakutana na Al-Merreikh kwenye mchezo wa raunsi ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika Dimba la Pele nchini Rwanda ambako Wasudan hao wamekita kambi.


Post a Comment

0 Comments