Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni (Pichani walioshikilia mfano wa Funguo)wameshiriki hafla ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji pamoja na uzinduzi na makabidhiano ya mitambo ya zimamoto na uokoaji iliyofanyika 13/05/ 2024 kikombo Jijini Dodoma.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni (Kushoto)ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali akiepo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Sillo wamehudhuria hafla hiyo.