Ticker

10/recent/ticker-posts

Soma Maneno mazito ya Hekima toka kwenye Ukurasa wa MNEC Richard Kasesela

Moja ya Mambo ambayo kwa tafiti mbalimbali humjenga na kumfanya mwanadamu awe bora sana ni kuweza kujizuia kuwa ni wakati gani useme,wakati gani usiseme na ni mahali gani unasemea..Leo katika safari yetu ya kujifunza kwa viongozi wetu wa Chama na Serikali tumepita katika ukurasa wa Instagram wa  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Ndg.Atufigwe Kasesela (Pichani) ambapo ameandika maneno mazito na ya hekima kubwa kuhusu faida ya kujifunza kunyamaza hasa kwa wenye mamlaka na hata wasio na mamlaka ambapo ameandika haya......

1. Kunyamaza wakati fulani maishani mwako siyo kipawa bali ni nidhamu
(1 Wathesalonike 4: 11).

2. Nyamaza unapohisi hasira
(Mithali 14:17).

3. Nyamaza unapokuwa huna taarifa ya kutosha au ukweli kuhusu unachotaka kusema (Mithali 18:13).

4. Nyamaza unapokuwa ni wakati wako kusikiliza na kujifunza
(Mithali 13: 1).

5. Nyamaza ukigundua kwamba maneno yako yataleta picha mbaya
(Mithali 17: 27).

6. Nyamaza ukijua kile unachotaka kusema kitaharibu jina na sifa ya mwenzio
(Mithali 16: 27).

7. Nyamaza ukijua utakachosema kitaharibu urafiki na kujeruhi mwenzako
(1Wakorintho 15: 33).

8. Nyamaza ukigundua kwamba utaaibika baadaye kwa sababu ya ulichokisema
(Mithali 8:8).

9. Nyamaza ukijua unachotaka kusema kitamdhalilisha Mungu, wewe mwenyewe au familia yako
(1Petro 2: 21-23).

10. Nyamaza ikiwa wakati ulio nao ni wakati wa kazi
(Mithali 14: 23).

11. Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, atajilinda nafsi yake na taabu
(Mithali 21: 23).

Mungu akupe neema ya kujenga nidhamu ya kunyamaza kwa maana maneno ya kinywa chako ni mtego kwako
(Mithali 6:2).

 

Post a Comment

0 Comments