Ticker

10/recent/ticker-posts

TARURA wajenga barabara mpya Mikoa ya Kigoma na Mwanza,Wasisitiza matumizi bora ya Barabara

 

Wakala wa Barabara  za Mijini na Vijijini TARURA  wamekamilisha ujenzi wa Barabara kadhaa mpya kwa Kiwango cha Lami katika Mkoa wa Kigoma na Jiji la Mwanza.
Akiongea ofsini kwake hivi karibuni Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema Hizo ni baadhi tu ya Barabara ambazo zipo katika mpango wa kufanyiwa matengenezo ikiwepo za viwango vya lami kwa mikoa mbalimbali kama ilivyopangwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na sasa utekeleazaji wa kazi za ujenzi kwa mwaka 2023/2024 umeanza hivyo kufikia mwakani wanaamini kazi nyingi zitakuwa kwenye hatua nzuri na nyingine zitakuwa zimefanyika kwa kliwango kikubwa.

Mhandisi Seff Amesema pia sehemu mbalimbali za nchi tayari madaraja na vivuko vimejengwa na mengine yako katika hatua mbalimbali za ujenzi ikiwa lengo ni kuhakikisha maeneo yanayozalishwa mazao na shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi zinafikika bila kikwazo kwani TARURA Wanatekeleza kwa vitendo falsafa ya Serikali inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea wananchi maendeleo hasa walioko vijijini ambapo uzalishaji wa mazao unafanyika. 

Aidha kwa Kumalizia Mhandisi Seff amewataka wananchi ikiwepo Viongozi wote wa ngazi mbalimbali kuwa mabalozi wema wa miundombinu inayojengwa na TARURA kwani baada ya ujenzi wa Barabara hatua zinazofuata ni matumizi ya barabara hizo kwa usahihi ikiwepo kuepuka kuziba mitaro au kuharibu barabara kwa kupitisha uzito mkubwa au kuruhusu uharibifu wa aina yoyote wa barabara ikiwepo Taa za Barabarani au Kuifanya mitaro kuwa Majalala kwani lengo la Mitaro inayowekwa kwenye barabara mbalimbali ni kusaidia kuririrsha maji hasa kipindi cha mvua na siyo Vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments