Ticker

10/recent/ticker-posts

Soma Taarifa hii mpya ya Msanii Rose Mhando

Meneja wa Msanii Maarufu wa Nyimbo za injili nchini Rose Mhando Bw.Abel Makalla amesema Msanii huyo anatarajia kuzindua albamu mbili  ambapo moja itakuwa na nyimbo zake zilizowahi kuweka rekodi na nyingine mpya ambapo albamu hiyo ya nyimbo za zamani ameipa jina la best of Rose Mhando pamoja na nyingine mpya inayoitwa Amefanya zitakazozinduliwa kwa pamoja hivi karibuni.

Makala amesema wapenzi na Mashabiki wa nyimbo za injili wakae tayari kwa mapokezi kwani albamu zote mbili zimekamilika na maandalizi yanaendelea vizuri hivyo watapewa taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu uzinduzi rasmi wa kazi hizo zinazosubiriwa kwa hamu na watu wengi.


Post a Comment

0 Comments