Ticker

10/recent/ticker-posts

Duuh..Kumbe Huu ndio Ukweli Kuhusu Waziri Jerry Silaa,..Hatimaye CV yake Yawekwa Hadharani,Ni hii Hapa



 Na Thadei Ole Mushi

Wiki iliyoishia Rais Samia alifanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri na katika baraza Hilo jina jipya kwenye viunga vya Baraza Hilo liliibuka ambalo ni JERRY SILAA. Hutokea Mara chache sana mtu kuwa waziri Moja kwa Moja bila kupitia unaibu Waziri hasa kwenye nabadiliko madogo ya baraza la mawaziri. Kutokea kwa hili wengi wamepigwa butwaa lakini kiuhalisia ni sawa na kwamba Rais Samia ameivumbua dhahabu iliyokuwa imesahaulika Stoo. 

Jerry Silaa ni nani?

ELIMU

Kwa viongozi vijana walioko Bungeni nawaza kusema ndiye msomi kuliko wote kwa idadi ya vyeti, stashahada na shahada (Hon Jerry Silaa is the most accomplished , connected and well-schooled young politician in Tanzania.):-

1. Jerry Silaa kidato cha sita alifanya mitihani miwili , NECTA na Cambridge yote kwa Mchepuo wa PGM na alifaulu vizuri. 

2. Mwaka 2002-2005 aliikuwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha sayansi akisomea Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Electronic na Mawasiliano ( Bachelor of Science in Electronics Science and Communication) Shahada hii ni kama vile Computer Science pamoja na Computer Engineering na Telecommunications kqa pamoja. Ni moja kati ya wataalam wa mwanzo wa mifumo ya Tehama na moja michango yake Bungeni kuukosoa mfumo wa Taneps ulizaa matunda na sasa serikali imezidua mfumo wa nest. 

3. Kipindi hicho hicho 2002-2005 alisoma Cheti cha Sheria ( Certificate in Law) kinachotolewa na kitivo cha sheria cha chuo kikuu cha Dar es Salam.

4.Kipindi hicho hicho [2002-2005] akasoma cheti cha uhasibu na ukaguzi wa mahesabu ATEC II kinachotolewa na Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu NBAA. 

5. Mwaka 2011-2015 alisoma Shahada Mbili; amesoma Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara yaani Masters of business administration MBA iliyotolewa kwa program ya Maastritch School of Management ya uholanzi na Esami. Moja katiba ya MBA bora kabisa. 

6. Lakini wakati huo huo [2011-2015] alisoma Shahada ya sheria LLB chuo kikuu huria. 

7. 2016-2021 alipambana na shule ya sheria,moja kati ya shule ngumu sana nchini na 2021 akatunukiwa stashahada ya juu ya uwakili yaani post graduate diploma in legal practise akaapishwa kuwa wakili wa mahakama kuu. Kwa sasa anasoma Shahada ya uzamili ya sheria za kodi LLM in Taxation UDSM ambayo itakuwa ya tano!!!


SIASA

Kuna ambao hawajui lakini wako wanajisahaulisha Jerry Silaa kwa vijana wa Bungeni pamoja na kuanzia chini kwenye UVCCM lakini pia ameshika nafasi za juu sana kwa muda mrefu na zote za kuchaguliwa kwa kura kama ifuatavyo:-

1. Mwaka 2003 alichaguliwa Mbunge wa Kitivo cha Sayansi na Waziri wa Daruso wa michezo.

2. Mwaka 1998-2003 alikuwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM wa Tawi.

3. 2003-2008 Mwenyekiti wa UVCCM wa Kata ya Ukonga na Mjumbe wa Baraza la Mkoa wa Dar es Salaam na kina Shaweji Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

4. 2005 alichaguliwa kwa kura zaidi yaa 19,000 kuwa diwani wa kata ya Ukonga akiwa  na miaka 23 tu! 

5. Mwaka 2006 aligombea unaibu meya na akaanguka. Akajipanga upya na 2019 akibuka naibu Meya wa halmashauri ya manispaa ya ilala. 

6. Mwaka 2010 kata ya ukonga ikagawanywa na akagombea kata ya Gongolamboto na kushinda na baadae kushinda kiti cha umeya wa manispaa ya ilala na kuiongoza 2010-2015. 

Turudi kwenye chama; 

7. Jerry Silaa alichaguliwa kwa kura nyingi kwenye mkutano mkuu wa 7 wa CCM kuwa mjumbe wa NEC 2007-2012 akachagukiwa tena 2012 kwenye mkutano mkuu wa UVCCM na kuwa Mnec 2012-2017. Na akachaguliwa tena 2017-2022.

8. Mwaka 2012 ilimpendeza mwenyekiti Mzee Kikwete akampendekeza jina lake kuingia Kamati Kuu na alishinda kwa kishindo kuwa MCC 2012-2017. 

9. Ni mbunge wa Kuchaguliwa Ukonga 

Nafasi zake zote kwenye Siasa ni za kupambana kwenye ushindani wa Kura kwa Mara ya Kwanza kama sijakosea kakumbukwa na kuteuliwa kuwa waziri.

In a Nutshell (Kwa kifupi kabisa) nataka kusema nini?

 JERRY SILAA kwa sifa za kiuongozi kawapita watu wengi sana ambao walimtangulia kuingia kwenye baraza la Mawaziri. Tuchukuelie mfano wacheche tu ambao wana majina makubwa kuliko Jerry jambo ambalo kiuhalisia sio sawa:-

Nape (Wasifu wake kwenye uongozi)

MNEC 2002-2007, 2007-2012 wa kuchaguliwa. 

MNEC 2012-2017 wa kuteuliwa 

Mwenezi Taifa 2010-2015 na MCC wa kuteuliwa. 

2022-2027 MNEC wa Kuchaguliwa 

Mbunge 2015-2020 , Mbunge 2020-2025

Waziri 2015- 2018, 2021- mpaka leo.

Nafasi za Kuchaguliwa 2 nafasi za kuteuliwa 4 kwa maana hiyo huyu amewahi kusubiria matokeo kwenye kinyang'anyiro cha kushindana Mara mbili  tu. Njia zake za kiuongozi si za mapambano sana ni za kusubiri connection mzazi wake ana background nzuri kwenye Siasa.

January 

2010-2012 MNEC na MCC Katibu wa Suki wa Kuteuliwa. 

2012-2017 MNEC wa Kuchaguliwa 

2010-2015 Mbunge wa Bumbuli

2012 -2015 NW Mawasiliano 

2015-2020 Mbunge wa Bumbuli 

2020-2025 Mbunge wa Bumbuli

2015-2018 Waziri Mazingira 

2021- mpaka leo Waziri 

2022-2027 Mnec wa kuchaguliwa 

Nafasi za kuchaguliwa 4 Kati ya nafasi 9 na katika hizo nne tatu amegombea eneo moja Bumbuli kama mbunge. Huyu naye anakanyaga Ganda la Ndizi la mzee wake kuteleza tu…..

Mwigulu

2011-2012 MNEC Mwekahazina wa CCM wa kuteuliwa. 

2012-2015 Naibu katibu Mkuu CCM wa kuteuliwa. 

2012-2017 MNEC wa Kuchaguliwa 

2012-2015 NW

2015-2019 W

2020 W

2020-leo Waziri 

2022-2027 MNEC wa kuchaguliwa 

Ubunge kachaguliwa Mara mbili 

Nafasi za kuchaguliwa 4 kati ya nafasi 10 za kiuongozi. Mbili kachaguliwa Kule Iramba 

Mtanisaidia hapa kufanya tathmini ndani ya Chama cha Mapinduzi ni kijana yupi ni mbobezi zaidi kwa vyeo viwe vya kugombea au kuteuliwa. 

MRENGO 

Jerry Silaa Bungeni amekuwa akipigana sana na mifumo, haki za wafanyabiashara, machinga, Bodaboda, kodi na mengine. Kamati yake ya Uwekezaji imekuwa nyota kwenye kazi za Bunge na inaonyesha imemsogeza zaidi karibu na masikio ya Watanzania na kuonyesha uwezo wake.

MISIMAMO

Jerry Silaa ni mtu wa misimamo na mara nyingi imemchonganisha na viongozi .Aliwahi kumbishia JPM kuhusu Mabango na kugomea agizo la kuyatoa. Sababu yake ilikuwa mabango ni chanzo cha mapato cha halmashauri cha wafanyabiashara wakubwa na ukiyatoa utaumiza wanyonge kwa kodi nyingi. Pili halmashauri zina mikataba na waliyatoa watashtakiwa. Tumeona nchi yetu ikishtakiwa na kushindwa kwa maamuzi ya kibabe ya viongozi na hivi karibuni tumeona kina igenge na prof Mruma. 

Amewahi kusigana na Job Ndugai na kwenye kesi yake alipasua mitandao kwa kwenda na Vitabu kwenye sanduku. Alipoulizwa alijibu sheria ya haki kinga na madaraka ya Bunge ndio imempa hayo majukumu ya kubeba vitabu. 

Akasimamishwa Bunge, akavuliwa ubunge wa PAP aliporudi February kama Ndugai alivyoagiza akakuta Ndugai sio Spika na yeye akachaguliwa Mwenyekiti wa PAC. 

UTEUZI 

Uteuzi wake umeshtua wengi na umebadilisha msimamo wa siasa za Tanzania. 

Wengi walijua atateuliwa uNW Sasa ameteuliwa W Tena wa Ardhi Mfupa ulomshinda fisi. 

Wengi wanamngoja kwa hamu kuona atafanya nini?  Ataanza na lipi? Atanunuliwa kwa vipande vingapi vya fedha. Toka ateuliwe yuko kimya. Sijajua ataanza kazi lini. Ardhi migogoro kila kona. 

Ole Mushi

0712702602

Post a Comment

0 Comments