Ticker

10/recent/ticker-posts

Yanga Waonyeshwa Mwangaza wa Ushindi Mkubwa Rwanda

KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda ambaye amewahi kukipiga ndani ya timu za Simba na Yanga, Haruna Niyonzima, amesema mbali na mapokezi makubwa ambayo kikosi cha Yanga itayapata itakapotua nchini Rwanda, pia anaamini timu hiyo ina uwezo mkubwa wa kuifunga Al Merrikh.

Septemba 16, mwaka huu, Yanga wanatarajiwa kuvaana na Al Merrikhya Sudan, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa nchini Rwanda kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi.

Kwa vipindi vitatu tofauti, Niyonzima amewahi kuhudumu katika timu za Simba na Yanga, huku akifanikiwa kushinda makombe matano ya Ligi Kuu Bara ndani ya misimu mitatu mfululizo.

Akizungumzia mchezo huo, Niyonzima alisema: “Nafurahi kuona timu yangu ya Yanga inakuja hapa Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Merrikh, napenda kuwaahidi kuwa nitakuwa mstari wa mbele kuongoza mapokezi, lakini pia kuhakikisha Yanga inapata matokeo ya ushindi na kuondoka hapa wakiwa na tabasamu.”

 

Post a Comment

0 Comments