Ticker

10/recent/ticker-posts

Maandamano yaliyopangwa kufanyika J’tatu yapigwa marufuku

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatahadharisha wananchi kuhusu taarifa zinazozagaa kutoka kwa mtu mmoja kuwa kutakuwa na maandamano siku ya Jumatatu Juni 19, 2023 kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 17, 2023 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amesema kuwa taarifa ya mtu huyo anayodai kuwa aliifikisha Polisi, tayari amejibiwa kwa kuyapiga marufuku maandamano aliyokuwa anataka kuyaratibu.

Kamanda Muliro amesema wanamshauri mtu huyo kama ana jambo la msingi atumie vyombo mbalimbali vya kisheria anavyoweza kufika na kuwasilisha hoja zake bila maandamano ili haki zingine za wananchi za kufanya kazi wakiwa huru zisiingiliwe.

Amesema Jeshi la Polisi linawatahadharisha watu kutoshiriki hicho kinachodaiwa maandamano na badala yake wanawahimiza kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu.


“Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kwa mtu au kundi la watu linalotaka kuzusha taharuki kwa kuzuia watu wengine kufanya kazi zao,” amesema

Post a Comment

0 Comments