Ticker

10/recent/ticker-posts

Rasmi:Samia Suluhu Aagiza Walioisaliti CCM kufukuzwa Mara Moja..!!!

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika Mkoa Kaskazini (A) Unguja, kuwachukulia hatua stahiki wanachama ambao wanakisaliti na kuhujumu shughuli za kujenga CCM mpya.

Samia alitoa kauli hiyo wakati anafungua mafunzo maalum ya viongozi na watendaji wa CCM na jumuiya zake wapatao 556 katika ngazi ya matawi, wadi/tarafa na majimbo katika Mkoa wa Kaskazini (A) Unguja.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia chama kuimarisha shughuli zake kwa sababu kitakuwa na watu waadilifu na wenye nia ya kukisaidia kusonga mbele na kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao.

Alisisitiza kuwa wanachama na viongozi wa CCM kote nchini waendelee kuweka mipango na mikakati imara itakayowezesha chama kuendelea kupata ushindi mkubwa na kushika dola.

Mjumbe huyo ambaye pia ni Mlezi wa CCM katika Mkoa wa Kaskazini A Unguja alisema umoja na mshikamano miongoni mwa wananchama na viongozi ndio silaha madhubuti itakayowezesha chama hicho kuimarisha shughuli zake na kuongeza maradufu idadi ya wanachama nchini.


Alisema kwa sasa viongozi wanatakiwa kujielekeza katika kufufua na kuimarisha jumuiya za chama ambazo katika baadhi ya maeneo hazifanyi kazi vizuri ili zianze kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama.