Ticker

10/recent/ticker-posts

RASMI: RAIS wa Iran Afariki Dunia, Mabaki ya Helkopta Yapatikana

 

TEHRAN, Iran: RAIS wa Iran, Ebrahim Raisi amefariki dunia katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa Iran kufuatia ajali ya helikopta iliyotokea hapo jana.


Asubuhi ya leo Ikulu ya nchi hiyo imethibitisha kifo cha rais huyo na kueleza kwamba katika helikopta hiyo, Raisi aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Hossein Amirabdollahian, Gavana wa Mashariki ya Azerbaijan, walinzi wa rais na maafisa kadhaa. Taarifa hizo zinaeleza kwamba hakuna uwezekano wa watu hao pia kuwa hai.


“Ndege ya Rais yote imeteketea kwa moto katika ajali hiyo hivyo hakuna uwezekano wa waliokuwemo ndani ya ndege hiyo kuwa hai, wote wanahisiwa kufa” Kimeeleza kituo kimoja maarufu cha habari maarufu nchini humo.


Rais wa huyo amefariki akiwa na miaka 63 alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa awamu ya pili mwaka 2021.

Makamu wa kwanza wa Rais wa nchi hiyo Mohammad Mokhber anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo na anatakiwa aitishe uchaguzi mpya wa rais ndani ya siku 50.