Ticker

10/recent/ticker-posts

KOCHA Jurgen Klopp aagwa kwa heshima Liverpool

 KOCHA Klopp aagwa kwa heshima Liverpool

Mabao ya kipindi cha kwanza ya Alexis Mac Allister na Jarell Quansah yamemfanya Jurgen Klopp kumaliza kibarua chake cha kuinoa Liverpool kwa heshima.

Mashabiki wa Liverpool wamefurika kwenye Uwanja wa Anfield kumshukuru Klopp ambaye leo Jumapili, Mei 19, 2024 alikuwa akiwaongoza wababe hao wa Ulaya kwenye mchezo wa mwisho.

Tayari Klopp alishatangaza kuachana na Liverpool mwishoni mwa msimu ambao umefikia tamati leo, akitaka kutumia muda zaidi na familia yake.

Liverpool imemaliza Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Arsenal, kwa kuichapa Wolverhampton mabao 2-0. Katika mchezo huo Nelson Semedo alimaliza msimu kwa kulimwa kadi nyekundu na kuifanya Wolves kucheza pungufu.

Akiwa na Liverpool, Klopp amebeba mataji ya EPL, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Klabu Bingwa Dunia na Super Cup.


Post a Comment

0 Comments