Ticker

10/recent/ticker-posts

Yanga Hii Sasa Sifa, Waja na "Gamondi Day" Mwendo wa Vipara..Jionee hapa

 Yanga Hii Sasa Sifa, Waja na "Gamondi Day" Mwendo wa Vipara

Wakati Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu ya Yanga ikijipanga kuwavaa Dodoma Jiji katika mchezo wa mzunguko wa 28 Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mechi hiyo imetolewa kama heshima kwa Mwalimu Miguel Gamondi ambae ameiongoza Yanga kubeba Ubingwa wake wa 30.

Akizungumza Gamondi kuelekea mchezo huo amesema;

"Kesho tunasafiri majira ya saa nne asubuhi kuelekea pale mkoani Dodoma kucheza dhidi ya Dodoma Jiji. Mchezo huo utafanyika tarehe 22 Mei 2024. Mechi hii ya Dodoma tumeifanya mechi ya kushukuru benchi la ufundi. Hivyo itakuwa ni Gamondi Day

Kwenye Gamondi Day itakapofika dakika ya 30, wana Yanga wote tunapaswa kusimama kumpigia makofi Gamondi na benchi lake la ufundi kwa dakika moja. Tunampa heshima Gamondi kwa kutupatia ubingwa wa kishitoria mara ya 30"

Post a Comment

0 Comments