Ticker

10/recent/ticker-posts

DUUH:JEURI YA PESA,SHUHUDIA BIRTHDAY YA MTOTO WA ODAMA..NI BALAAH

Pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibwena Bongo ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Msasani Beach, Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo shughuli nzima ilikuwa imeandaliwa kama harusi ambapo kwa mujibu wa waandaaji iliteketeza mamilioni ya shilingi yanayodaiwa kumwagwa na baba mtoto lakini mwenyewe akaingia mitini.
Kilichoweka rekodi kwenye sherehe hiyo ni pamoja na vinywaji na misosi ambayo waalikwa walikula na kunywa hadi wakasaza huku mama mlezi wa wasanii, Mama Loraa akivua saa yake ya mkononi ya dhahabu na kumpa mtoto huyo ambaye alikuwa akilia.
Baadhi ya mastaa waliotinga ni pamoja na Kajala Masanja, Halima Yahya ‘Davina’, Salome Urassa ‘Thea’, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Mama Loraa, Zubery Mohamed ‘Niva’, Jimmy Mafufu, Herieth Chumila na wengine wengi ambao walifanya sherehe kufana vilivyo ambapo walikula na kunywa hadi baadhi yao wakawa ‘bwi’

Post a Comment

0 Comments