Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan akipozi na mdada.
MSHINDI wa
Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan ameonywa na
mashabiki kuwa makini na akina dada kwani mamilioni ya shilingi
alizokuja nazo zitawafanya wampapatikie kwa lengo la kumchuna.
Wadau
mbalimbali waliokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar Jumatano hii kumsubiri wakati akiwasili kutokea Johannesburg,
Afrika Kusini, walisema umaarufu na pesa alizonazo utamfanya kuwa
kimbilio la masista duu.
“Milioni
510 ni pesa nyingi sana kwa kijana mdogo kama Idris, akijilegeza na
kuziona nyingi, muda si mrefu tutasikia hadithi tu, isije ikawa kama
yule mwingine nani sijui yuko wapi siku hizi,” alisema Skata Malcom,
akimuulizia aliyewahi kushinda shindano hilo miaka ya nyuma, Richard
Bezuidenhout.
Idris aliyetegemewa kuwasili Jumatano jioni, alishinda shindano hilo baada ya kukaa katika mjengo huo kwa muda wa siku 63 na hivyo kuwa Mtanzania wa pili kushinda shindano hilo. Richard alipewa kitita cha dola laki moja mwaka 2007.