Ticker

10/recent/ticker-posts

KUMBE ASILIMIA 75 YA WANAWAKE/WASICHANA WANAKIRI SIMU ZINAVUNJA MAHUSIANO YAO..

Kama simu yako ya mkononi haikatiki kiganjani mwako muda wowote, inaweza ikawa inaharibu uhusiano wako na umpendaye. Wanasaikolojia wamesema kuwa watu wengi kwa sasa wanalazimika kushindana na smartphone za wapenzi wao kupata attention. 

Utafiti uliofanywa, umebaini kuwa robo tatu ya wanawake wanaona kuwa smartphones zinaingilia maisha yao ya mapenzi na kupunguza muda ambao wangetumia kuzungumza au kuwa karibu na wapenzi wao. Wanasayansi wamedai kile walichokiita ‘technoference’ kina madhara makubwa kama migogoro mingi, kupunguza quality ya uhusiano, kupunguza mridhisho wa maisha na hatari kubwa ya msongo wa mawazo. 

Utafiti huo ulifanywa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha jimbo la Pennsylvania, Marekani na mwingine wa chuo kikuu Brigman Young University cha Utah na kuhusisha wanawake 143.

Asilimia 62 walisema teknolojia imeingilia muda waliotumia pamoja na wapenzi wao na theluthi moja wakisema boyfriend zao waliangalia smartphone wakati wakizungumza. 

Wanasayansi hao wameshauri kuweka simu silent na kutokuwa nazo muda wote ili kuwa na muda wa kufocus kwa mpenzi wako. “Kama unataka kuangalia kitu muhimu, toa maelezo kwanza na kisha angalia simu yako.

Na pia usijitetee pale mpenzi wako akionesha kukerwa na tabia yako ya kuangalia sms au kucheza games mara kwa mara – ni njia ya yeye kusema kuwa angetaka kuconnect na wewe moja kwa moja.