Ticker

10/recent/ticker-posts

DUUH:HEBU MWONE MWANAMKE ALIYEKATWA MASIKIO NA MME WAKE KISA WIVU WA KIMAPENZI


Mwanaume mmoja Ndomo Mwandu Mkoani Katavi amemkata mkewe Agnes Sikazwe masikio kutokana na wivu wa kimapenzi.





Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea Novemba 8 mwaka huu majira ya saa sita usiku nyumbani kwa wanandoa hao.





“Kabla ya ugomvi wanandoa hao walikua na ugomvi wa amara kwa mara uliokuwa umedumu kwa muda mrefu na chanzo cha ugomvi huo ni kwamba mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine kijijini hapo.





Siku ya tukio wanandoa hao walikuwa wamelala lakini baadaye mwanaume alimvizia mkewe akiwa usingizini na kumkata masikio huku akilalamika bado anaendelea na mahusiano na mwanaume mwingine.





Baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele kuomba msaada kwa majirani.