Ticker

10/recent/ticker-posts

Kumbe Hiki ndicho Kilicho Sababisha Kifo cha Msanii Costa Titch

 Familia ya Mwanamuziki Costa Titch Yatoa Ripoti Kuhusu Kilicho Sababisha Kifo chake

Familia ya Costa Titch Wametoa Taarifa Rasmi Kuhusu Ukweli Juu ya Sababu ya Kifo Cha Mpendwa wao!! Hii Hapa ni Taarifa Hiyo Kwa Tafsiri Isiyo Rasmi.

Costantinos Tsobanoglou Au aliyejulikana Kama Costa Titch, Ambaye Alikuwa mwanamuziki Na Dancer, Baada ya Kutotarajiwa Kuanguka Mwezi March Akiwa Anafanya show Katika Tamasha La Utra Music, alitangazwa kufariki March 11, 2023.

Kutokana na uvumi, team yetu na Familia tukishirikiana na mtaalam Wa magonjwa (Maalum Ambao wamesomea Kuangalia Taarifa Za Ugonjwa Kwa kutumia human tissue Au damu Au Hata mkojo) Ili Kujua Ukweli Wa chanzo Cha Kifo chake. Uchunguzi Wa Maiti yake uliofanywa umegundua mkandamizo Mkubwa Katika Moyo wake Ambao haukujulikana Ikiwa umechanganywa na msongo Wa Mawazo na uchovu. Haya yamepelekea mapigo yasiyo Sahihi ya Moyo Na kuchochea Mstuko Ambao ulichukua Maisha yake.

Watu Wengi Zaidi wamekuwa wakitiwa Moyo Kwa Maisha aliyoyaishi Costa Titch, akiacha alama Katika ulimwengu Wa Mziki. Katika Kipindi hiki Cha maombolezo, tunatoa shukrani zetu za dhati Kwa fans Kwa Mapenzi Yao ya na support isiyoyumba. Tuendelee kumuenzi Kwa Pamoja Kwa alichotuachia.

Rapper Costa Titch Wa Africa Kusini, alifariki Dunia Akiwa Jukwaani, Alipokuwa akitumbuiza, Msanii Huyu alianguka, akaamka na Kuanguka Tena na kupewa Msaada. Costa Titch alitamba na Kibao Chake Maarufu Cha Big Flexa Ambacho Mpaka Sasa kina Watazamaji Million 98 YouTube.

Post a Comment

0 Comments