Ticker

10/recent/ticker-posts

Eng.Victor Seff:TARURA Imerejesha mawasiliano maeneo yote yaliyoathiriwa na Mvua,Asisitiza utunzaji wa Miundombinu


Mtendanji mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amesema tayari TARURA imerejesha mawasiliano ya Miundombinu ya maeneo mbalimbali ya nchi yaliyoathiriwa na Mvua ambazo zinaendelea kunyesha mikoa mbalimbali ya nchi.

Aidha Mhandisi Seff aliyasema hayo jana Jijini Dodoma ambapo ametolea mfano maeneo yaliyoathirika wiki chache zilizopita kwa Mikoa ya  Dar es Salaam,Morogoro na kwingine  ambapo Madaraja na Barabara kadhaa ziliathiriwa na mvua kubwa tayari TARURA waemesharejesha hali ya kawaida kwa uakarabati wa Haraka uliofanywa na Wataalamu wake.

Mhandidi Seff ameendelea kuwasisitiza wananchi kutunza miundombinu ya barabara na Vivuko jambo ambalo ni moja ya njia ya kufanya miundombinu hiyo idumu muda mrefu kwani hata mvua zinaponyesha madhara yake yanakuwa madogo zaidi.

Ikumbukwe katika jiji la Dar es Salaam Daraja la Mbopo,Salasala na mengine yalikatika huku yakisababisha wananchi kukosa mawasiliano kwa masaa kadhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ila kwa sasa maeneno yote hayo yapo katika hali ya kawaida na inasemekana iliwachukua TARURA siku 2 hadi 5 tu kukamilisha kazi ya ujenzi wa madaraja hayo maeneno mbalimbali.



Post a Comment

0 Comments