Ticker

10/recent/ticker-posts

DC Grace Kingalame ataka watoto wenye sifa kuanza shule mara moja Nyang'wale,awaonya wazazi wanaowatumikisha na kuwazuia

 


Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita Mhe.Grace Kingalame 

Mkuu wa Wilaya ya NYANG’HWAALE Mkoani Geita Mhe.Grace Kingalame amewaonya Wazazi na walezi wanaowatumikisha watoto katika shughuli nyingine badala ya kuwapeleka shule. 
Kingalame amesema hatomvumilia mzazi au mlezi yeyote atakayemnyima mtoto haki ya kusoma kwa kumpeleka kuchunga ng’ombe, kwenye shughuli za Madini na kwingineko. 

DC Kingalame amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa ya kuhakikisha mtoto wa Kitanzania anapata elimu bora katika mazingira mazuri na bila malipo, hivyo kama msimamizi mkuu wa shughuli za serikali wilayani NYANG’HWALE hatomvumilia yeyote atakayezivuta juhudi hizo nyuma. 

Aidha amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuwapelekea miradi mingi ya maendeleo ikiwemo katika sekta ya elimu ambapo hivi karibuni wamekamilisha shule mpya ya Sekondari iliyogharimu takribani shilingi Milioni 584 na Januari hii watoto wameanza kusomea hapo.

 

Post a Comment

0 Comments