Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff ametembelea miundombinu ya barabara za Kijiji cha Msomera ambapo ni moja ya eneo maalumu lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuwahamishia wafugaji waliokuwa wakiishi katika hifadhi ya Ngorongoro.
Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa Makazi ya
Wafugaji Kanali S.E Mihayo amempongeza Mhandisi Seff kwa ushirikiano mkubwa
unaotolewa na watendaji wa TARURA na akimpongeza Meneja wa Wilaya ya Handeni
Mhandisi Eng. Judica Makyao kwa kujitoa kikamilifu kuhakikisha barabara
zinafunguliwa na kupitika katika eneo la mradi.
Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Hendeni Mhandisi Judica Makyao alimuambia Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff kuwa, mtandao wa barabara katika Kijiji cha Msomera unajumla ya kilometa 986, ambapo jumla ya kilometa 186 za barabara zimekamilika kuchongwa na kilometa 24 zimewekewa kifusi na changarawe. Alieza kuwa Mkandarasi yupo eneo la kazi na kuendelea na ufunguzi wa barabara pamoja na ujenzi wa Makalavati 10 katika Kijiji cha Msomera
Mhandisi Seff alimpongeza Kanali Mihayo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya Ujenzi wa Makazi ya Wafugaji na kumuahidi TARURA itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha ujenzi wa barabara unakuwa wa viwango vilivyokusudiwa ili kufikia adhima ya malengo mazuri ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Comments