Ticker

10/recent/ticker-posts

Viongozi UWT Kilimanjaro waitaka jamii kuwa wakweli kupinga ukatili, UWT Hai, DC Mkalipa nao watoa neno

 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro Elizabeth Minde 

 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro Elizabeth Minde ameitaka jamii hususani wanawake kubadilika kitabia ikiwa ni kujenga dhana ya kusema kweli pale wanapotendewa vitendo vya kikatili.

Ameyasema hayo katika kikao cha UWT kilichofanyika ukumbi wa flomena na kuwakutanisha wanawake kutoka katika kata mbalimbali wilayani hai mkoani Kilimanjaro.

Katika kikao hicho viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wameshiriki akiwemo mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Amiri mkalipa, mwenyekiti wa UWT Happiness Eliufoo madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa mbalimbali.

Minde ambaye alikuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo amempongeza mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Amiri Mkalipa kwa kuunga mkono ajenda ya maendeleo kwa wanawake.

Hata hivyo ameiomba jamii kuripoti vitendo vyote vya ukatili pale vinapotokea katika jami inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kushirikiana kupiga vita vitendo hivyo viovu.

Mkuu wa wilaya Hai mkoani Kilimanjaro Mhe.Amiri Mkalipa 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Hai mkoani Kilimanjaro Mhe.Amiri Mkalipa ameonyesha hamasa katika utendaji wake ikiwa ni pamoja na kuwaahidi wa kina mama kutoa ushirikiano wake katika mahitaji yao.

Pia amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto ili kuepukana na vitendo vya ukatili vinavyoripotiwa kila mara katika ofisi yake.

Amesema wale wote wanaofanya vitendo hivyo hatosita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine

Mwenyekiti wa UWT wilaya Happiness Eliufoo

Nae mwenyekiti wa UWT wilaya Happiness Eliufoo amesema wanapambana na ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha watoto na wanawake wanakuwa salama

Hata hivyo amewataka wanawake kutafuta kiini cha matatatizo ya ukatili kwani pia yanaathiri ushiriki wa wanawake katika uongozi.

Katibu wa CCM Wilayani Hai Ndugu Mussa Ballo 

Katibu wa CCM Wilayani Hai Ndugu Mussa Ballo alipopokuwa akisisitiza umuhimu wa kupambana na ukatili wa kijinsia na kuahidi wao kama Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwa bega kwa bega na jamii katika kupinga vitendo hivyo.

Imeandikwa na 

Masama Blog- Hai

Post a Comment

0 Comments