Ticker

10/recent/ticker-posts

Diamond Platnumz Afunguka asema "Siachi Mpaka Waombe Poo, Ndo Kwa Kwanza Tumeanza"

 


Msanii @diamondplatnumz aliwahi kusema "Siachi pengo mpaka waombe poo" kwenye moja ya line kupitia freestyle ya 'All The Way Up' wimbo wa French Montana.

Sasa hiki ndicho kinaenda kutokea baada ya kusema kuwa nyimbo zitaendelea kutoka back to back mpaka mashabiki wenyewe wasema inatosha.

Tamko lake hilo limeambatana na shukrani zake kwa mashabiki ambao wanampa nguvu ya kuendelea kuibeba Tanzania mabegani kupitia muziki.

"Ahsante kwa upendo, kama ambavyo nilisema, ndio kwanza tumeanza. Ni Mvua ya Mawe hadi kuhakikisha mashabiki wenyewe mnasema jamani inatosha".

Post a Comment

0 Comments