Ticker

10/recent/ticker-posts

WHO yakubali Mitishamba itafutwe Afrika kupambana na Covid19


Hii ni moja ya Top stories za wiki hii ambapo Shirika la Afya duniani WHO na kituo cha udhibiti wa magonjwa kwenye Bara la Afrika CDC wameanzisha mpango wa kuangalia uwezekano wa kutumia dawa za mitishamba katika kupambana na janga la virusi vya corona.

Jopo hilo jipya la ushauri litaunga mkono Nchi za Afrika katika majaribio ya kitabibu, utafiti mwingine na utengenezaji wa dawa nyingine za  kienyeji  wakati hivi sasa janga hili likiendelea kuitesa dunia kwa kasi katika baadhi ya sehemu ikiwemo Afrika ambapo Wagonjwa waliothibitishwa katika bara hilo wakikaribia 750,000 huku nusu yake ikitajwa kutokea South Africa.


Matshidiso Moeti

Taarifa ya WHO imesema dawa za asili zina faida nyingi na bara la Afrika lina historia ndefu ya matumizi yake ambapo Mkuu  wa  WHO Afrika Matshidiso Moeti amesema hata hivyo utafiti unapaswa kuwekwa katika misingi ya kisayansi.

Nchi kadhaa zilionesha shauku baada ya Rais wa Madagascar kutangaza dawa ya mitishamba kama sehemu ya taifa hilo la  kisiwani kupambana na janga la virusi vya corona ambapo wakati huo Rais Magufuli ndio alikua Rais pekee aliyehimiza Watu kuomba Mungu pamoja na kujifukiza kwa dawa za mitishamba.