Ticker

10/recent/ticker-posts

Askofu Gwajima Ashindwa Kura za Maoni CCM Jimbo la Kawe.....Mshindi ni Furaha Dominic Jacob

Zoezi la kura za maoni katika Jimbo la Kawe Dar es salaam ndani ya CCM, limemalizika na matokeo yametolewa ambapo Furaha Dominic Jacob ameongoza kwa kupata kura 101.

Jimbo hilo lilikuwa na jumla ya watia nia 170 huku wajumbe wenye sifa za kupiga kura walikuwa ni 475.

Dominic Jacob amefuatiwa na Angella Kiziga ambaye amepata kura 85 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Askofu Josephat Gwajima 79.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta ameshika nafasi ya 4 kwa kupata kura 61, huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kabla ya kuhamia CCM mapema mwaka huu Vincent Mashinji amepata kura 2.