MKAZI WA MBAGALA RANGI TATU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUUZA DAWA ZA KULEVYA

  Masama Blog      
Mkazi wa Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam,  Abuu Kimboko (43) akitoka katika kahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashitaka ya kukabiliwa na tuhuma za  kujihusisha  na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroine na utakatishaji fedha. 

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
MKAZI wa Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam,  Abuu Kimboko (43) pichani amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za  kujihusisha  na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroine na utakatishaji fedha. 

Akisoma hati ya mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally, Wakili wa Serikali, Elia Athanas akisaidiana na Tuly Helela, amedai kati ya Desemba Mosi na 29, 2019 huko Mbagala Zakhem wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Kimboko alijihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 273.45.

Imeendelea kudaiwa kuwa, katti ya Desemba  Mosi na 29, mwaka jana maeneo ya jiji la Dar es Salaam, mshitakiwa alijipatia sh. 990,000 huku akifahamu kuwa fedha hizo ni mazalia ya biashara ya dawa za kulevya.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza  kesi za uhujumu uchumi hadi itakapopata kibali kutoka kwa Mkurugenzi  wa Mashitaka  nchini (DPP).

Kwa mujibu wa upande wa  mashtaka, upelelezi  wa kesi hiyo uko mbioni  kukamilika  hivyo, aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine  ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa alirudishwa rumande kwa sababu haina dhamana kisheria.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30l6IWj
via
logoblog

Thanks for reading MKAZI WA MBAGALA RANGI TATU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUUZA DAWA ZA KULEVYA

Previous
« Prev Post