RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WANNE, AWAASWA KUWAHI KWENDA KUTUWAKILISHA

  Masama Blog      
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
"IKIWEZEKANA ndani ya wiki moja muwe mmeshaenda kwenye nchi ambazo mnatuwakilisha", hayo yameelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwaapisha Mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali Ikulu jiji i Dar es Salaam leo".

Mabalozi walioapishwa ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Namibia, Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, na Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi Tanzania Nchini Nigeria.

"Na nchi tulizowapeleka wote nyinyi wanne ni nchi ambazo (very potential) katika kujenga uchumi wa Taifa letu, nendeni mkiamini mnawakilisha taifa na taifa lenye mwelekeo mpya katika maendeleo ya watu wake",alisema Rais

Hata hivyo Rais Magufuli amewakumbusha Mabalozi hao majukumu ya Taifa letu katika nchi za SADC ikiwa nchi walizochaguliwa kuwakilisha ni wanachama wa SADC katika kujenga maendeleo na uchumi wa kisasa.

"Kasimamieni uchumi, kasimamieni taifa, kahakikisheni mnatengeneza ajira'employment' kwa watanzania katika nchi mnazowakilisha, najua mkienda kusimama vizuri mtafanya vizuri". Amesema Rais Dkt. Magufuli.

Hata hivyo amewaasa wakamtangulize Mungu katika kazi zao kwani Mungu ndiye kila kitu, na matumaini yake kuwa watafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Rais Magufuli amewaonya tabia ya kwenda kuaga kwa viongozi mbalimbali wa serikali kwa nia ya kupoteza siku kadhaa ikiwa yupo hapa nchini badala ya kwenda kule walikopangiwa kuwakilisha Taifa.

"Tunataka unapoteuliwa na kuchapa kazi na hii ndio maana ya hapa kazi tuu, na mimi ninauhakika mtaweza tuu mtaweza tuu sana ". Amesema Rais, Dkt. Magufuli.
Mabalozi walioapishwa Ikulu leo, jijini Dar es Salaam na Rais Dkt John Pombe Magufuli, wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa Umma, pichani kushoto ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi (Afrika Kusini) '  Dkt. Modestus Francis Kipilimba ( Namibia), Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah ( Zimbabwe) pamoja na Dkt. Benson Alfred Bana ( Nigeria).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2tWJ3z9
via
logoblog

Thanks for reading RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WANNE, AWAASWA KUWAHI KWENDA KUTUWAKILISHA

Previous
« Prev Post