Ticker

10/recent/ticker-posts

NI MBOWE TENA KUIONGOZA CHADEMA KWA MIAKA MITANO, LISSU KUWA MAKAMU MWENYEKITI

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amechaguliwa tena katika nafasi hiyo baada ya kupata kura 886 sawa na 93.5% dhidi ya mpinzani wake Cecil Mwambe aliyepata kura 59 sawa na 6.2%. 

Wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara) walikuwa wagombea wawili,Tundu Lissu na Sophia Mwakagenda, Lissu amepata kura 930 sawa na 98.8% huku Mwakagenda (aliyetangaza kujitoa akiwa ukumbini) akipata kura 11 sawa na 1.2%.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Zanzibar ambayo ilikuwa na mgombea mmoja, Said Issa Mohamedi, ameshinda kwa kura za ndio 839 sawa na asilimia 88.7,kura za hapana zilikuwa ni 95 sawa na asilimia 10 na zilizoharibika 12 sawa na asilimia 1.3.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuliwa na wanachama na wajumbe wa chama hicho kwaajili ya uchaguzi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2sH1l6S
via

Post a Comment

0 Comments