Hatima ya Trump kusalia madarakani mikononi mwa Bunge la Seneti

  Masama Blog      
 Donald Trump amekuwa rais wa tatu katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya matumizi mabaya ya madaraka, hatua inayompeleka moja kwa moja katika kesi dhidi yake itakayoamua ikiwa atabakia mamlakani au la.

Bunge la Wawakilishi (Kongresi) lilipigia kura mashtaka mawili - kwamba rais alitumia vibaya mamlaka yake na kwamba alizuia shughuli za Bunge hilo.

Kura zote zilipigwa kulingana na mirengo ya vyama huku karibu wabunge wote wa chama cha Democtrats wakipiga kura kuunga mkono ashtakiwe huku Republican wakipinga kura hiyo.

Wakati kura ilipokua inapigwa, Bwana Trump alikuwa akihutubia mkutano wa wafuasi wake.

Aliuambia umati wa watu waliokua wamekusanyika katika eneo la Battle Creek, jimboni Michigan kwamba: "Wakati tunabuni ajira na kupambana kwa ajili ya Michigan, wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto katika Congress wamejawa na wivu na chuki na hasira kubwa, unaona kile kinachoendelea."

Ikulu ya White House ilitoa taarifa inayosema kuwa rais "anaimani kwamba atasafishwa na tuhuma zote" katika kesi hiyo kwenye Bunge la Seneti.

Vikao vya Jumatano vya Kongresi vilianza kwa wajumbe wa wa chama cha rais Trump cha Republican kuomba kwanza utaratibu wenyewe wa siku upigiwe kura wakiwa na nia ya kuleta usumbufu.

Hiyo ilifuatiwa na kura juu ya sheria zitakazotumiwa kwa ajili ya uchunguzi, mchakato uliochukua muda wa saa sita za mjadala wa wabunge wa pande mbili juu ya uhalali, umuhimu na uzito wa mashtaka mawili dhidi ya Trump. 
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2r6cQEr
via
logoblog

Thanks for reading Hatima ya Trump kusalia madarakani mikononi mwa Bunge la Seneti

Previous
« Prev Post