JESHI LA POLISI LAWATAKA MADEREVA WA MABASI YANAYOKWENDA MIKOANI KUWA WAANGALIFU

  Masama Blog      

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Fortunatus Muslim akizungumza na madereva wa mabasi yanayokwenda mikoani. 
 
Kamanda Muslim amewataka madereva kuwa waangalifu katika kuhakikisha usalama wa abiria hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutokana na uzoefu wa huko nyuma kwamba kipindi kama hiki hutokea ajali nyingi. 
 
Muslim pia aliwataka madereva kuzingatia suala la afya na kuwasisitiza kutosimamisha magari sehemu zisizo rasmi kwaajili ya abiria kujisaidia, amesema suala hilo maarufu kama kuchimba dawa ni kosa kisheria na sio salama kwa wananchi kujisaidia vichakani na wanaweza pia kuwasababishia ajali kutokana na madereva kusimamisha magari maeneo ambayo sio salama, badala yake amewataka kusimamisha magari maeneo ambayo yamejengwa vyoo na yameandaliwa rasmi kwa abiria kupata huduma hiyo.PICHA NA JESHI LA POLISI.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Z7PgDR
via
logoblog

Thanks for reading JESHI LA POLISI LAWATAKA MADEREVA WA MABASI YANAYOKWENDA MIKOANI KUWA WAANGALIFU

Previous
« Prev Post