Ticker

10/recent/ticker-posts

WANANCHI BUTIAMA WAHOFIA MADAWATI YA JINSIA KUVUNJA NDOA


Mwandishi wetu Butiama Mara

Baadhi ya wakazi wa Butiama Mkoani Mara wameiomba  serikali kuongeza nguvu katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili kutokomeza tatizo hilo ambalo limeonekana kuwa sugu Mkoani Mara huku baadhi ya wanaume wakidai ufunguzi wa madawati hayo yatavunja ndoa kwani baadhi ya wanawake watakuwa jeuri.

Wametoa ombi hilo wilayani Butiama baada ya Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Sirro kufungua ofisi ya dawati la jinsia ambapo kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema licha ya madawati ya jinsia kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ukatili lakini pia wanawake wamekuwa wajeuri kwa kuwa wanajua wataenda kushitaki

Akizungumza na wananchi hao Mkuu huyo wa jeshi la Polisi amesema mfumo dume bado unasumbua wanaume wa Mkoa wa Mara na kwamba jeshi la polisi haliwezi kuvumilia mambo yaliyopitwa na wakati lazima washugulikiwe kwa nguvu zote.

"Salamu zangu kwa wanaume ubabe haulipi wakati Rais Magufuli akiniteua alikuwa na maana yake huwa nikisema jambo sitanii sasa wewe baba jaribu uone"amesema Sirro

Aidha amesema ng'ombe hana nafasi ya kuruhusu ulatili kwa mwanamke eti kwa sababu alitolewa mahari ya ng'ombe na kwamba ndiyo maana madawati yameanzishwa nchi nzima kulinda haki za wanawake na watoto lakini pia amewataka wanawake wasizidi wakasababisha balaa.

"Kina mama lindeni watoto wenu wazazi wangu wasingenilinda leo nisingekuwa IGP hujui mtoto wako atakuwa nani baadae na nyie wababa msiwarubuni watoto wadogo nendeni kwa wakubwa wenu wamejaa tele na nyie watoto wa kike msilubali kurubuniwa na vitu vidogo vikaharibu ndoto yako ukiona kuna viahashiria vya mtu mzima kukurubuni au kukutaka kimapenzi nenda kwenye dawati"alisema IGP Sirro

Naye Mkurugenzi wa  jukwaa la utu wa mtoto Koshuma Mtengeti amesema kutokomeza ukatili wa jinsia kutaleta maendeleo kwani wanawake watajishughulisha kikamilifu kujenga uchumi na kuwa uzinduzi wa dawati hilo utatoa chachu kukusanya rasilimali na kuweka nguvu pamoja kutokomeza ukatili.

"Tunapata faraja sana kuona IGP anaongoza mapambano kutokomeza ukatili nnamini tutashinda cha msingi wananchi tutoe ushahidi pale ambapo unahitajika hili ni janga letu sote" amesema Mtengeti

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu UNFPA Jackqueline Mahon amesema lengo ni ifikapo mwaka 2030 vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia viwe vimetokomezwa.

Pia ameipongeza serikali ya Tanzania na jeshi la polisi kwa jitihada kubwa inayofanya kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinatokomezwa. 
 Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Sirro akifungua ofisi ya dawati la jinsia na Watoto Butiama mkoani Mara,huku wadau mbalimbali wakijitokeza kushiriki tukio hilo.

Picha ya pamoja


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2DtgPh6
via

Post a Comment

0 Comments