Ticker

10/recent/ticker-posts

Wanariadha mbio za Nyika Taifa waiahidi NCAA

Na Mwandishi Wetu, Arusha
WANARIADHA watakaoshiriki mashindano ya mbio za Nyika za Taifa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Magereza Moshi, mkoani Kilimanjaro wameahidi kufanya makubwa zaidi.
Kufanya vizuri kwenye mashindano hayo kutawapa fursa ya kushiriki mashindano ya mbio za Nyika za Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Denmark Machi 30, mwaka huu.  Wakizungumza kwenye mazoezi yaliyofanyika viwanja vya Magereza Arusha wanariadha hao walisema chini ya mdhamini wao Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA),wamejaa tumaini la kufanya vizuri zaidi.
Mwanariadha kutoka timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Anjelina Daniel aliwashukuru NCAA kwa kuwadhamini ambapo amekuwa na wakati mzuri zaidi wa kufanya mazoezi.   “Ninawaahidi mashindano ya Nyika Moshi nitashika namba ya kwanza hapa nimekuwa wa pili,” alisema Anjelina.
Kaimu Meneja wa Uhusiano NCAA Joyce Mgaya alisema Mamlaka ya Ngorongoro ilitambua fursa ya uzalendo kwenye mchezo huo na mingine.“Hili ni jukwaa linaloweza kutangaza vivutio vya utalii. Tuliona vizuri kuungana na RT kuwatia moyo wachezaji, tunaamini watakuwa mabalozi wazuri wa utalii,” alisema Mgaya.
Naye Katibu Mkuu wa RT Wilhelm Gidabuday aliwashukuru NCAA kwa kuwashika na mkono.


from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2G9qEE6
via

Post a Comment

0 Comments