Ticker

10/recent/ticker-posts

NEWS ALERT: MAPIPA 75 YA MAFUTA YA DIZELI YAKAMATWA BANDARI BUBU KAWE BEACH,KINONDONI JIJINI DAR

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) akikagua mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyokamatwa katika bandari bubu eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam leo katika operesheni yake ya kupambana na magendo, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, ufukwe kwa ufukwe, mtu na mtu ili kukomesha biashara hiyo.
Mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyokamatwa katika bandari bubu eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam leo katika operesheni yake ya kupambana na magendo, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, ufukwe kwa ufukwe, mtu na mtu ili kukomesha biashara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) akikagua mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyokamatwa katika bandari bubu eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam leo katika operesheni yake ya kupambana na magendo, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, ufukwe kwa ufukwe, mtu na mtu ili kukomesha biashara hiyo.


Serikali wilayani Kinondoni, jijini Dar es S Salaam, leo imefanikiwa kuvamia bandari bubu ikiwa imehifadhi shehena ya mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyoingizwa nchini kinyemela ili kukwepa kodi. 

Mafuta hayo yamenaswa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo aliyeongozana na maofisa wa TRA, EWURA na vyombo vya usalama. 

Mfuta hayo yamekutwa yamehifadhiwa katika nyumba moja iliyopo Mtaa wa Kolekole, Kawe Beach, yenye namba KAW/MZN/1542. 

Chongolo alisema, mafuta hayo yamethibitika kwamba ni mafuta ya dizeli na Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta (EWURA) na kwamba pia wamejiridhisha ni dizeli na yameingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu. 

Alisema mapipa yako 75 ni sawa na lita 17,000 ambapo thamani yake kwa tathimini ya wali ni zaidi y ash.milioni 20. Ofisa Mfawidhi wa Kitengo cha Kuzuia Magendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania b(TRA) Hafidhi Abdallah, alisema wali tarifa ya kuwepo shehena ya mafuta katika eneo hilo tangu Januari 31 mwaka huu katika nyumba hiyo. 

Alisema wahusika walifanikiwa kutoroka na wanaendelea kuwasaka na kwamba mafuta hayo yatataifishwa .


from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2D99uT0
via

Post a Comment

0 Comments