Ticker

10/recent/ticker-posts

VIJANA NA MAPENZI YAO.. UMEIPATA YA WASICHANA 17 WALIOKUTANA HOSPITALI KUMUONA BWANA MMOJA?HEBU SOMA HAPA

CB74quDWMAESkhc
Tumezoea kukutana na story za watu kufumaniana majumbani.. kwenye nyumba za kulala wageni na kwingineko, huyu bwana imemkuta Hospitali.. japo huwezi kuliita ni fumanizi lakini jinsi ambavyo kagonganisha wanawake zake 17 ni ishu mtu wangu.
Yuan alipata ajali ya gari, akawa amelazwa Hospitali March 24.. sasa kama kawaida si kuna ndugu jamaa na marafiki wakapata taarifa kwamba ndugu yao kapata ajali, wakawa wanakuja kumjulia hali.. mbaya zaidi ikawa pale ambapo wasichana 17 ambao wote ana uhusiano nao walifika kwa pamoja Hospitali tena bila kujuana.
yn
Baadhi ya wanawake na waandishi wakizungumza na Daktari.
Wang Fang ni mwanamke aliyezaa na Yuan mtoto mmoja, amesema hakuwahi kuhisi kama mume wake ana uhusiano na wanawake wengine, kwa sasa kajua hilo amekubali matokeo.. kasema hana haja tena kumpenda mzazi mwenzake.
Mwanamke mwingine Xiao Li nae alikuwa kwenye uhusiano na jamaa kwa zaidi ya miezi 18, alipata uchungu kusikia mpenzi wake amepata ajali.. alipokutana na wasichana wengine Hospitali wote wamekuja kumuona Yuan ilibidi uchungu wote umuishe.. ameona asahau kabisa suala la ndoa na mpenzi wake huyo.
Chinas-Romeo-Car-crash-Casanova-caught-out-at-hospital (1)
Yuan
Wanawake hao wamefungua group lao Facebook, eti kwa sasa wanajadili kuona jinsi ambavyo jamaa huyo amewachezea wote 17 kwa wakati mmoja na wasijue.

Post a Comment

0 Comments