Ticker

10/recent/ticker-posts

IDRIS SULTAN ASEMA AMEKOMA KUWEKA WAZI MASUALA YAKE YA KIMAPENZI

idris na wemaMshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, Hotshots Idris Sultan, amesema misukosuko aliyoipata baada ya kuweka wazi maisha ya mahusiano yake na maklia wa filamu, Wema Sepetu, imetosha.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Idris amesema kwa sasa hawezi tena kukaa mbele ya mwaandishi wa habari na kuzungumzia maisha yake ya mapenzi.
“Masuala ya mapenzi yangu sasa hivi sitaki kuyazungumzia kabisa, kwa sababu sasa hivi sitaki kiwe ndiyo kipaumbele changu, nina kazi nyingi sana naweza kuzifanya na focus yangu ipo kwenye vitu vikubwa na vya umuhimu. Kwa hiyo siyo kitu ambacho nitakuwa nakiongelea kivile,” alisema Idris.
Pia Idris aliizungumzia sababu ya kuamua kufanya hivyo na kama kuna matatizo yametokea kati yake na Wema Sepetu.
“Matatizo yalitokea, tukapatana na sasa tupo sawa, hakuna tatizo,” alisema Idris.