Ticker

10/recent/ticker-posts

Henock Inonga Kuondoka SIMBA Mwisho wa Msimu Huu wa Ligi

 Henock Inonga Kuondoka SIMBA Mwisho wa Msimu Huu wa Ligi

Henock Inonga Baka ni miongoni mwa wachezaji ambao tutawakosa kwenye ligi kuu msimu ujao.

Beki huyo wa Simba yupo katika nafasi nzuri ya kuitumikia FAR RABAT ya Morocco  chini ya kocha Nassredine Nabi.

Inonga Baka mwenyewe amewataarifu viongozi juu ya kuondoka ndani ya Simba baada ya msimu kumalizika.

FAR RABAT msimu ujao wanamalengo ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na taarifa kutoka Morocco 🇲🇦 ni kwamba Inonga Baka na FAR RABAT wamefikiana makubaliano kwaajili ya usajili wa nyota huyo ambaye atalipwa mshahara wa Mara mbili na robo ya ule anaolipwa sasa ndani ya Simba.

Post a Comment

0 Comments