Ticker

10/recent/ticker-posts

Jionee hapa RC SENYAMULE alivyofanya hafla ya IFTAR na kufuturisha makundi mbalimbali pamoja na wana dodoma jijini humo


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule April 05, 2024 amefanya hafla ya Iftar kwenye viwanja vya makazi yake yaliyopo Barabara ya Faharani, Kata ya Kilimani Jijini Dodoma. Iftar hiyo iliyoandaliwa na Ofisi yake imelenga kufuturisha makundi mbalimbali kwenye jamii ya Wana Dodoma kama ilivyo desturi ya Mkuu huyo.

Senyamule amewahusia waumini wa dini ya Kiislam na Wanadodoma kwa ujumla kudumisha upendo na mshikamano hasa katika kipindi hiki wanapokwenda kukamilisha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kusherehekea sikukuu ya Eid El fitr ili kuimarisha Amani na usalama katika Mkoa wao.





Post a Comment

0 Comments