Ticker

10/recent/ticker-posts

TBT:Rais Samia ,Rais Mwinyi, Balozi Nchimbi,Pandu Kificho na Waziri Silaa ,Maisha ni Hatua

Picha ya Kumbukumbu ikiwaonyesha Wanachama  wa Chama Cha mapinduzi baada ya kikao cha Kamati kuu ya CCM miaka ya 2012-2013 katika ukumbi wa White House Dodoma ambapo picha hii  ilipigwa miaka zaidi ya 10  iliyopita na  katika picha hii kutoka kushoto yupo aliyekuwa Waziri na Naibu Waziri katika Wizara mbalimbali Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa sasa,Mjumbe wa Kamati Kuu na pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba ambaye kwa Sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,Mzee Pandu Ameir Kificho ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu,Spika wa Baraza la wawakilishi pamoja na Bunge la Katiba, Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya  CCM,na sasa ni Katibu Mkuu wa CCM  Aliyewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala,Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Jerry Silaa ambaye kwa Sasa ni Mbunge wa Ukonga na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Cha Kujifunza ni kwamba Omba Sana Dua na Sala kwa Mwenyezi Mungu na usikate Tamaa katika Malemgo yako,Uuadilifu,Uwajibikaji na Uvumilivu  ni Silaha kubwa za Kukufikisha katika Malengo yako na Hakuna Ajuaye Kesho yake Bali Mwenyezi Mungu.





 


Post a Comment

0 Comments