Ticker

10/recent/ticker-posts

CCM Dodoma Wampongeza RC Senyamule na Waziri Silaa kwa utekelezaji mzuri wa Ilani,Wasisitiza kauli nzuri kwa wananchi toka kwa watumishi

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Dodoma chini ya Mwenyekiti Ndg. Alhaj Adam Kimbisa Jijini Dodoma tarehe 19 Disemba 2023 ilikutana  kwa kikao cha kawaida cha kujadili hali ya kisiasa ,uchumi na mambo mbalimbali yanayohusu ustawi ndani ya Mkoa huo kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2023.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kikao hicho Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dodoma Ndg.Jawadu Mohamed amesema Halmashauri hiyo imeelekeza kuwa Watumishi wote wa serikali ndani ya Mkoa huo kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, kusikiliza kero pamoja na kutotoa lugha za maudhi na matusi kwa wananchi.

" Halmashauri kuu imeelekeza kwa Watumishi wote wa serikali ndani ya Mkoa wa Dodoma kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, kusikiliza kero lakini kutotoa lugha za maudhi na matusi kwa wananchi " Amesema Ndg.Mohamed

Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde akiongea katika kikao hicho kilichofanyika mwezi uliopita jijini Dodoma.

Ndg.Mohamed amesema Halmashauri hiyo imeazimia kwa kauli moja ya kumpongeza Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya maendeleo ambayo amekuwa akifanya ndani ya Mkoa ya kuendelea kustawisha Makao Makuu ya nchi.

Pia,imetoa Pongezi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (Mb) kwa kupokea maelekezo kutoka kwa Mhe.Raisi Dkt.Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ya kushughulikia migogoro ya ardhi ndani ya Mkoa wa Dodoma kupitia kliniki maalumu ya kutatua changamoto hizo.

Kadhalika,Halmashauri Kuu imetoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (pichani) Mhe.Rosemary Senyamule kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) kwa kuzunguka kwenye miradi na kufanya ukaguzi

Post a Comment

0 Comments