Ticker

10/recent/ticker-posts

Mbunge Thadayo na Mtendaji Mkuu TARURA Wakagua ujenzi wa Mkalavati 16 na Barabara ya Kisangara Wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro


Pichani ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff  na Mbunge  wa Jimbo Mwanga Mhe. Joseph Tadayo walipotembelea ujenzi wa Makalavati Kumi na Sita (16) yanayojengwa kwenye Barabara ya Msuya yenye urefu wa kilometa 13.8 iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro .



Akizungumza katika ziara hiyo ya Ukaguzi wa Miradi ilnayofanywa na Mtendaji Mkuu wa TARURA kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Miradi ya TARURA Meneja wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Nicholaus Francis  amesema kwa Mradi huu unatekelezwa na muungano wa Wakandarasi wawili   Wazawa (M/S Casco Construction na Bronze Tech Company Ltd) ambapo unaendelea vizuri ambapo  Mtendaji Mkuu aliwataka Wakandarasi hao kumaliza kazi kwa Wakati kabla ya vipindi vya mvua kuanza mwezi Machi mwaka 2024.


Pichani pia katika ziara yake mkoani Kilimnajaro Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff wa kwanza kulia alifanya ukaguzi wa mradi wa matengenezo ya barabara ya Kisangara kwenda Shighatini yenye urefu wa Kilometa 25 inayotengenezwa na Kikundi Maalum cha kijamii (Special Group) kiitwachoa Muhako Engineering (Labour base) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro tarehe 02.01.2024. 


Mtendaji Mkuu alifurahishwa na ushiriki wa Vikundi vya Kijamii katika utekalizaji wa Miradi ya Ujenzi na Matengenezo ya Barabara. Mkurugenzi wa ufundi wa Kikundi cha Muhako Stephen Mkeni alimueleza Mtendaji Mkuu wananchi katika eneo la mradi wameshirikishwa vyema kwenye kazi zinazoendelea kwa kuwapatia ajira. 

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu alilisitiza Halmashauri ya Mwanga kuhamasisha ushiriki wa vikundi vya Kijamii kwenye kazi za ujenzi na Matengenezo ya Barabara ili kufika asilimia 30 ya bajeti zinazotengwa kwa kazi za matengenezo ya barabara zitakazotekelezwa na vikundi maalumu vya kijamii kila mwaka ili kuwawezesha kiuchumi na kuondokana na umasikini.


Post a Comment

0 Comments