Ticker

10/recent/ticker-posts

BREAKING NEWZ:Hivi ndivyo Waziri Huyu alivyokutwa akila Mihogo kwa Mama Ntilie,Asema ndio Maisha aliyokulia

 

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jerry Silaa ambaye pia ni  Mbunge wa Ukonga amekutwa akiwa anafurahia jambo na mmoja wa wananchi wake jimboni Ukonga ambaye ni mfanyabiashara ya chakula yaani Mama Lishe au maarufu Mama Ntilie huku akila kipande cha Muhogo wakati  alipokuwa katika Ziara ya kukagua Utekelezaji wa Ilani  ya CCM na ahadi za Serikali kwa wananchi ambapo alipoulizwa na Mwandishi wa Habari Hii anajisikiaje amesema kwake ni jambo la furaha sana kuona wananchi wanajitengenezea kipato kwa njia mbalimbali za halali ambapo Moja ya Vyakula anavyopenda yeye ni vya Asili ikiwepo Mihogo na Magimbi kwani amekua katika maisha hayo tangu utoto kwani Shuleni na nyumbani kwa wazazi wake Mihogo kilikuwa ni chakula muhimu na bora ndo maana aliamua kupitia hapo kununua na kula kama wateja wengine.

Mbunge wa Ukonga na Waziri wa ardhi Mhe. Jerry Silaa akimsikiliza Mama Lishe huyu ambaye ni Mmoja wa wapiga Kura wake ambaye pia mama lishe huyo amempongeza kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Taznania Mhe.Samia Suluhu Hassan na kumteua kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwani wao kama wananchi wa Ukonga wanaamini ni bahati kwao na ina tija kubwa kuwa na waziri ambaye anaamini atakuwa mmoja wa watatuzi muhimu wa Migogoro ya Ardhi Nchini ikiwepo jimbo la Ukonga.

Waziri Jerry Silaa akiondoka kwa Mama lishe huyo baada ya kumsikilza na kupata mihogo kama Chakula chake cha  mchana huku akiisifia kwa kusema watu wengi hawajui kama mihogo ni moja ya chakula bora na kinacholiwa sana na watu wengi hasa maeneo ya mijini na vijijini kwani yeye tangu akiwa shule ya msingi,sekondanri hata vyuo kwake Mihogo ni moja ya chakula anachokipenda sana

Post a Comment

0 Comments