Januari 5, 2024, Dodoma
Na. Raymond Mtani BMH
Imeelezwa kuwa
kuzungumza kwa njia ya simu kwa muda mrefu kinaweza kuwa chanzo
mojawapo cha kupoteza usikivu. Hayo yamesemwa na Leonard Tibihika, Mtaalamu wa
Upimaji Usikivu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) katika mahojiano
maalumu kuhusu huduma za
uchunguzi wa
Usikivu Hospitalini hapo, leo Januari 5, 2024.“isitafsirike vibaya, si kila
anayeongea na simu anahatarisha usikivu, bali yule anayetumia muda mrefu
kuongea na simu, kwa sababu mgandamizo wa sauti inayoingia sikioni
ukiendelea kwa muda mrefu huathiri Ngoma ya Sikio” Alisema
Tibihika.
Watu wengine
waliyoko katika hatari ya kupoteza usikivu ni wale wanaofanya kazi katika
mazingira ya kelele, alisema Mtalaamu huyo akitolea mfano, wafanyakazi wa viwandani
na wanaokesha kwenye klabu za muziki, na wale wenye shughuli katika masoko.“changamoto
anayoweza kukutana nayo mtu anayepoteza usikivu ni kutogundua mapema kuwa
usikivu wake hauko katika kiwango cha kawaida, akachukua hatua kwa sababu
usikivu hupungua polepole wakati mwingine hadi ambiwe na wengine”
Tibihika.
Kuchelewa
kugundua kuwa usikivu unapotea, au kugundua na kutochukua hatua za kuchunguzwa
ili kutibiwa husababisha watu wengi kufika Hospitali wakiwa katika hatua mbaya
kiasi cha kuhatarisha kupoteza usikivu kabisa. Taarifa za Vituo vya Udhibiti na Kukinga Magonjwa (CDCs) zinadokeza
kuwa,
Watoto na Vijana wadogo milioni 5.2 na watu wazima milioni 26 hupoteza uwezo wa kusikia kutokana na kuwa kwenye mazingira ya kelele. Katika moja ya tafiti kuhusu kupoteza usikivu kwa matumizi makubwa ya simu uliyobandikwa katika tovuti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), unathibitisha kuwa
matumizi ya
zaidi ya dakika 60 kila siku yanaweza kuathiri usikivu wa binadamu
ndani ya miaka
5.
Tibihika, anatoa
wito kwa watumiaji wa simu kwa muda mrefu, kuchukua hatua za kujikinga,
pamoja na kuhakikisha wanafanyiwa uchunguzi wa usikivu angalau mara mbili ndani
ya miezi 12. Hospitali ya Benjamin Mkapa, ni miongoni mwa Hospitali tatu za
serikali nchini zinazotoa huduma za uchunguzi wa usikivu kwa kufanya vipimo vya aina
zote, asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopoteza usikivu hubainika kuwa na
tatizo la kupasuka Ngoma ya Sikio.
0 Comments