Ticker

10/recent/ticker-posts

Naibu Waziri David Kihenzile amwakilisha Profesa Mbarawa Mahafali ya 39 ya Chuo cha NIT

 

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David Mwakiposa Kihenzile amehudhuria mahafali ya 39 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji yaliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete.

Mahafali hayo yamefanyika sambamba na uzinduzi wa kitabu kilichoeleza historia ya Chuo hicho.

Akiongea Katika Mahafali hayo Naibu Waziri David Kihenzile alisema:

Nimetoa Salam za Serikali kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi Mh Profesa Makame Mbarawa nikieleza uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan  na kuwaahidi wanajumuia ya Chuo hicho na watanzania kwamba Wizara yetu itaendelea kutenga fedha kila mwaka ili kukiweezesha kutoa wataalam waliobobea katika Eneo la Uchukuzi.


Rai ya Mgeni Rasmi Mhe. Jakaya Kikwete katika mahafali ya NIT ni juu ya Uongozi wa Baraza la Chuo pamoja na maboresho yanayofanywa na Uongozi uzingatie Msingi wa kuanzishwa ikiwemo kuzalisha wataalam wa astashahada na stashada katika uchukuzi

Post a Comment

0 Comments