Ticker

10/recent/ticker-posts

Breaking: Dkt. Tulia Ashinda nafasi ya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)...Soma hapa ilivyokuwa


Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson ameshinda kwa kishindo na kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Dkt. Tulia amepata ushindi wa kura 172 za Tanzania, huku Somalia wakipata kura 11, Senegal kura 59 na Malawi wakipata kura 61 katika Mkutano huo wa 147.

Uchaguzi huo umefanyika leo nchini Angola katika Jiji la Luanda na katika maelezo yake wakati akiomba kura jana, Dkt. Tulia aliwaahidi kusimamia misingi ya Umoja kwa kuongeza Ufanisi, Uwajibikaji na Uwazi.

Ikumbukwe Miezi Michache iliyopita katika Blogu hiiya Masama Blog tulichapisha wasifu wa Mhe.Dkt Tulia Ackson pia tukaelezea kwa nini Dkt Tulia Akson ni Chaguo Bora kwa wapiga Kura na wajumbe wa Uchaguzi huo kwa sasa,Hongera sana Mhe.Dkt Tulia Ackson,Timu nzima ya Masama Blog iko nawe Bega kwa Bega kwatika kuiwakilisha Tanzania katika Nafasi Hii uliyoshinda.

Post a Comment

0 Comments