Ticker

10/recent/ticker-posts

Waziri Angellah Kairukli acharuka Sakata la Vichanga Mapacha ''Kutolewa Macho" Wawili Wasimamishwa Kazi Tabora

 

Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Mhe.Angellah J. Kairuki amesema amepokea kwa masikitiko makubwa malalamiko ya mzazi Kisaka Mtoisenga Mkazi wa Ushikola wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Tabora, kufuatia Watoto wake mapacha waliozaliwa katika Kituo cha Afya Kaliua na baada ya muda mfupi kufariki na kukutana na dosari (wameng’olewa macho, kukatwa ulimi na kuchunwa ngozi kwenye paji la uso) baada ya Wazazi kukabidhiwa miili yao mnamo tarehe 10 Mei, 2023.

Kufuatia taarifa hiyo, OR - TAMISEMI kupitia Halmashauri ya Wilaya ya
Kaliua imewasimamisha kazi Wauguzi wawili wa Kituo cha Afya Kaliua ili kupisha uchunguzi na imekabishi kwa Jeshi la Polisi suala hili ili waendelee na chunguzi wa tukio hili.

Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe.Angellah Kairuki amendelea kuwakumbusha Wataalam katika Vituo vya kutolea huduma za Afya chini kote kuzingatia miongozo na taratibu za Kitaaluma zilizowekwa na Serikali wakati woe wanapohudumia Wananchi.

Post a Comment

0 Comments