Ticker

10/recent/ticker-posts

Senegal yatawala Soka la Afrika, yashinda tena Kombe Jingine la AFCON

 

Kwa mara nyingine tena Senegal inaendelea kutawala soka la Afrika, jana usiku Senegal imechukua ndoo ya AFCON U17 2023 baada ya kuipasua Morocco 2-1 kwenye mchezo wa Fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika nchini Algeria.

Kwa hiyo sasa Senegal ni mabingwa wa mashindano yote ya Afrika kwa timu za Taifa za wanaume! Kwa kifupi ni kwamba ndoo zote zipo kwao, AFCON, AFCON U20, CHAN, Beach Soccer na sasa AFCON U17.

2021 AFCON [senior] 🏆
2022 BSAFCON [Beach Soccer] 🏆
2023 CHAN 🏆
2023 AFCON U20 🏆
2023 AFCON U17 🏆

Ukiangalia muunganiko wa mafanikio ya soka la Senegal hauishii tu kwa timu yao ya wakubwa [senior team] ambayo inaongozwa na akina Mane, Koulibaly, Mendy lakini mafanikio yao yameshuja hadi kwa timu za vijana.

Nini kimejificha nyuma ya mafanikio ya soka la Senegal? Swali hili linaweza kuwa gumu au jepesi sana.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Augustin Senghor [Rais wa Shirikisho la Soka Senegal] anatajwa sana kama mtu ambaye yupo nyuma ya mafanikio ya Senegal.

Pekeyake hawezi bila Serikali ya Senegal chini ya Rais wa nchi Macky Sall. Serikali ina nafasi kubwa ya kutengeneza mazingira ya mafanikio ya michezo kwa ujumla wake hususan mchezo wa soka ambapo tunaizungumzia Senegal kama taifa lililofanikiwa zaidi kwa sasa barani Afrika.

Kwenye kila mashindano ya Afrika waliyoshiriki wamebeba ubingwa, hii haitoikei kwa bahati mbaya wala kwa kubahatisha! Huwezi kubahatisha kwenye kila sehemu.

Maana yake wamejiandaa na falsafa yao inafanya kazi, ukiangalia kila timu [Senior team, U17, U20 na CHAN] zote zilikuwa na walimu wake lakini kiwango cha ushindani ni kilekile.

Kwa hiyo Senegal wanaweza kutamba kwa muda fulani kwenye soka la Afrika ikiwa nchi nyingine hazitachukua hatua kwa sababu kizazi cha Mane kikiondoka bado wana mtaji mkubwa wa vijana wa U20 na U17 ambao wanaweza kuchukua nafasi.

Sky is the limit for Senegal 😍

Post a Comment

0 Comments